By James Gashumba,
EANA
Arusha, Oktoba 15,
2013 (EANA)-- Wakuu wa majeshi ya polisi ya nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) wamekubaliana kuanzisha vutuo mbalimbali vya mafunzo vyenye
ubora katika kanda ili kuvijengea uwezo wa kukabiliana na changamoto
mbalimbali.
Vituo hivyo
vitajikita katika masuala mbalimbali yakiwemo ya unyanyasaji wa kijinsia,
udhibiti wa majanga, uchunguzi wa makosa ya jinai,udhibiti wa silaha haramu na
utii wa sheria.
Vituo hivyo vitatoa
mafunzo mbalimbali kwa maafisa wa majeshi ya polisi wa nchi za EAC kwa lengo ya
kuwajengea uwezo kiutendaji.
Mkutano wa wakuu wa
majeshi ya polisi uliofanyika Kampala, Uganda mwishoni mwa wiki umekubaliana
kwamba nchi hiyo iwe mwenyeji wa Kituo cha Polisi Jamii huku Rwanda kuwa Kituo
cha Mafunzo na Udhibiti wa Unyanyasaji Kijinsia.
''Dhana hiyo inahusu
yule mwenye msingi mzuri katika nyanja fulani ambako sote ndiko tunaweza
kuanzia,'' Mkuu wa Jeshi la Polisi la Uganda (IGP), Kale Kayihura alieleza.
Mratibu wa Polisi wa
Rwanda wa Masuala ya Uchunguzi wa mwili wa Binadamu,Wilson Rubanzana alisema
moja ya vituo hivyo kitakuwa makao makuu ya Jeshi la Polisi mjini Kigali nchini
mwake.
Alisema vituo vingine
vitakuwa katika Chuo cha Taifa cha Polisi cha Musanze,Kaskazini ya Rwanda na
Chuo cha Mafunzo ya Polisi, Mashariki mwa Rwanda.
Mkutano huo pia
uliichagua Kenya kuwa kituo cha masuala ya Anga na Makosa ya Jinai wakati
Tanzania itakuwa mwenyeji wa kituo cha Polisi wanamaji na Udhibiti wa Sheria.
Burundi kutokana na
uzoefu wake wa masuala ya kushughulika na migogoro itakuwa mwenyeji wa kituo
cha Udhibiti wa majanga na silaha haramu.
Uganda kwa upande
wake itakuwa mwenyeji wa kituo cha Uchunguzi wa mwili wa binadamu.
Jg/lc/ni
0 comments:
Post a Comment