Mtuhumiwa namba 8 katika kesi ya mauaji ya Mfanyabiashara wa Madini ya
Tanzanite Erasto Msuya, aliyekamatwa hivi karibuni Ally Musa "Majeshi"
akipelekwa katika chumba cha mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshi kwa
ajili ya kuunganishwa na watuhumiwa wenzake katika kesi hiyo.
Mtuhumiwa namba mbili, Shaibu Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama
Mredi(38) anayetuhumiwa kushiriki Mauaji ya mfanyabiashara wa madini
Erasto Msuya wakipelekwa katika jengo la mahakama.
Mmoja wa askari akijaribu kutoa maelekezo kwa mtuhumiwa wa mauaji ya
mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya wakati akielekea chumba cha
mahakama ya hakimu mkazi mjini Moshi.
Ndugu wa marehemu Erasto Msuya wakiwa nje ya jengo la mahakama ya
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya
wakitolewa katika chumba cha mahakama mara baada ya kuahirishwa kwa
shitaka linalo wakabili.
Watuhumiwa wa kesi ya mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto Msuya
wakitolewa katika chumba cha mahakama mara baada ya kuahirishwa kwa
shitaka linalo wakabili.
Mtuhumiwa namba mbili, Shaibu Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredi
(38) anayetuhumiwa kushiriki Mauaji ya mfanyabiashara wa madini Erasto
Msuya, akisaidiwa kupanda katika gari mara bada ya kuahirishwa kwa
shitaka linalo wakabili.
MTUHUMIWA “Muhimu” katika kesi ya mauaji ya Bilionea wa madini ya
Tanzanite, Erasto Msuya (43), Ally Mussa “Majeshi” (42) amepandishwa
mahakamani LEO katika Mahakama ya hakimu mkazi Moshi, mkoani
Kilimanjaro.
Mtuhumiwa huyo aliyekamatwa Oktoba 8, mwaka huu, alinaswa mkoani Kigoma
akijaribu kutorokea nchini Burundi baada ya kufanikiwa kukimbia mitego
ya polisi katika mikoa ya Arusha, Dodoma na Mwanza na kurudishwa mkoani
kilimanjaro ambapo jana aliunganishwa katika kesi ya Mauaji ya Msuya.
Akisoma Mashtaka yanayomkabili Mtuhumiwa huyo mbele ya Mahakama ya
Hakimu Munga Sabuni, Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Serikali, Janet
Sekule alisema Mshtakiwa huyo pamoja na wenzake Saba, wanashtakiwa kwa
kosa la kuua kwa kukusudia kinyume cha kinyume cha kanuni namba
16,kifungu cha 196 ya sheria za makosa ya jinai, “Kinyume cha sheria ya
makosa ya jinai, kanuni ya 16, kifungu cha 196, Ally Mussa au kwa jina
lingine Majeshi, walimuua Erasto Msuya katika maeneo ya Mjohoroni, njia
panda ya Arusha na KIA kwa kumpiga risasi,” alisema Sekule.
Aidha baada ya kusoma maelezo ya shtaka hilo, upande wa Jamhuri,
ukiwakilishwa na Wakili wa Serikali, Janet Sekule iliiomba Mahakama ya
Hakimu Sabuni kuipa muda kuweza kukamilisha upelelezi ambapo kesi hiyo
iliahirishwa hadi Oktoba 28, mwaka huu, itakapo tajwa tena.
Ally Mussa “Majeshi”, anayedaiwa kuwahi kulitumikia Jeshi la kujenga
Taifa (JKT), kabla ya kufukuzwa anaungana na Sharif Mohamed Athuman (31)
mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, Shaibu
Jumanne Saidi maarufu kama Mredi (38), mkazi wa Songambele Wilaya ya
Simanjiro.
Wengine ni Joseph Damas Mwakipesile maarufu kama Chusa (36),
mfanyabiashara wa madini na mkazi wa Arusha, Jalila Zuberi Said (28),
mkazi wa Babati, Sadiki Mohammed Jabir ‘Msudani’ au ‘Mnubi’(32), mkazi
wa Dar es Salaam na Lang’ata wilayani Hai na Karim Kihundwa (33) mkazi
wa Kijiji cha Lawate Wilaya ya Siha na Mussa Juma Mangu (30), mkazi wa
Shangarai kwa Mrefu mkoani Arusha.
Hata hivyo Mwandishi wa Habari hizi alishuhudia kesi hiyo ikisomwa
katika hali ya utulivu tofauti na ilivyozoeleka kwani katika mara zote
kesi hiyo ilipofikishwa Mahakamani hapo kulikuwa na umati mkubwa wa watu
wakiwemo ndugu za Marehemu Erasto Msuya.
Mfanyabiashara Erasto Msuya, aliuawa Agosti 7, mwaka huu majira ya 6:30
mchana kwa kupigwa risasi 13 kifuani, kando ya barabara kuu ya Arusha–
Moshi katika eneo la Mjohoroni, Wilaya ya Hai, karibu na Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
Credit: kijiwe
0 comments:
Post a Comment