ARUSHA
Mkutano wa kumi wa mwaka wa kamati za bunge za fedha kwa nchi zilizoko kusini mwa jangwa la sahara sadc umefanyika leo jijini arusha ambapo mgeni rasmi alikua waziri mkuu wa tanzania mizengo pinda.
Waziri pinda alifungua mkutano huo na kuzitaja mada ambazo
zitazungumziwa ikiwemo mfumo wa kuziwasilisha bajeti ili kujua namna fedha zinavyotumika mahusiano miongoni mwa nchi washirika na hali ya mazingira kwa ukanda wa sadc.
Naye mwenyekiti wa sadcopac sifo makama amesema ili nchi iwe na maendeleo yenye manufaa ni vizuri bajeti inayotengwa iwezeshe mipango mingine ya maendeleo kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Wakati huohuo waziri pinda amezindua jumuiya ya afropac ambayo itasaidia kuzishauri nchi washirika namana ya kutumia fedha wanazozipata.mwenyekiti wa kamati za bunge za serikali kwa Tanzania mhe. Zitto kabwe amehudhuria mkutano huo kwa niaba ya bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania.

0 comments:
Post a Comment