Home » » Watendaji wa vijiji na kata wilaya ya Longido watafutiwa dawa

Watendaji wa vijiji na kata wilaya ya Longido watafutiwa dawa


Mbunge wa Jimbo la Longido, Lekule Laizer

Na.ashura Mohamed,Arusha


Kutokana na
watendaji wa kata na vijiji kukithiri kwa ubadirifu wa fedha za serikali na
wananchi, halmashauri ya wilaya ya longido imejipanga kukabiliana na tatizo hilo
ili kuokoa fedha ambazo zimekuwa zikipotea bila kuleta maendeleo yoyote katika
kata na vijiji husika.

Akizungumza
katika baraza la madiwani diwani wa kata ya Tinga Tinga,Sabore Moimollet
alisema kuwa wakati umefika sasa kwa halmashauri hiyo kupitia idara ya utumishi
kuwafukuza kazi watendaji wa kata na vijiji ikiwa ni pamoja na kuwachukulia
hatua kali za kisheria.

Alisema kuwa
watendaji wengi ni walevi na wamekuwa wakitumia fedha hizo vibaya kwa kuwa
wanafahamu kuwa hakuna mkaguzi yeyote anayefuatilia akaunti hizo hali
inayosababisha kuzorota kwa maendeleo ya vijiji,kata kutokana na fedha hizo
kutoelekezwa katika kutatua kero mbalimbali zinazoikabili jamii.


Aidha
alisema kuwa idara ya utumishi sasa ilifanyie
kazi swala hilo na kuhakikisha kuwa wakaguzi wanafuatilia akaunti hizo
mara kwa mara ili kuhakikisha fedha hizo hazipotei bila sababu ya msingi na
pindi ubadirifu unapojitokeza hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Kwa upande
wake Mbunge wa Jimbo la Longido, Lekule Laizer alisema kuwa ili kukabiliana na
tatizo hilo madiwani wa halmashauri hiyo waorodheshe majina ya vijana
waliomaliza elimu ya kidatp cha nne na sita wenye uwezo ili wakapitiwe mafunzo
maalum ya uongozi na utawala ili wajengewe uwezo na kuweza kusaidia vijiji na
kata zinazoizunguka halmashauri hiyo.

Alisema kuwa
pindi vijana hao watakapopatiwa mafunzo hayo itawasaidia katika kufanya kazi
kwa uadilifu hali ambayo itachangia kwa kiwango kikubwa maendeleo ya vijiji na
kata hali ambayo itawasaidia halmashauri hiyo kupata maendeleo na hatimaye
kutumia vizuri fedha hizo na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa
vijiji na kata zilizopo katika wilaya hizo.

Kwa hisani ya Full Shangwe blog

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa