Home » » TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KONGAMANO LA 26 LA KISAYANSI LITAKALOFANYIKA JIJINI ARUSHA

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KONGAMANO LA 26 LA KISAYANSI LITAKALOFANYIKA JIJINI ARUSHA

Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya NIMR Dk. Mwele Malecela (kulia)  akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu



 Kongamano la Kisayansi litakalofanyika kuanzia  tarehe 16-19 April, 2012 katika
ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC mjini Arusha.
Kongamano hilo litatoa fursa kwa wanasayansi,
wakufunzi, watoa maamuzi na watunga sera; waandishi wa habari na jamii kwa
ujumla; kupata taarifa za matokeo ya tafiti mbalimbali za afya ya binadamu na
kubadilishana uzoefu kuhusu ubooreshaji wa afya ya jamii na utafiti wa afya kwa
ujumla.


Kauli mbiu ya kongamano hili kwa mwaka huu wa 2012 ni
“Mafanikio
ya Sekta ya Afya katika kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia: Kuelekea
2015”
.
Kongamano
litafunguliwa rasmi tarehe 16 April 2012 – na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania DAKTA MOHAMED
GHARIB BILLAL.
Kongamano hili la
Kisayansi ambalo limekuwa likiandaliwa kuanzia mwaka 1982 na Taasisi ya Taifa
ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu–NIMR;
litafanya makongamano madogo sita yatakayoendeshwa kwa kuzingatia kaulimbiu
ambayo inalenga kutathimini Mafanikio ya Sekta ya Afya katika kutekeleza
Malengo ya Maendeleo ya Milenia: Kuelekea 2015
Makongamano hayo
madogo yatajadili masuala mbalimbali yakiwemo
1)
Magonjwa yanayoambukiza na
yasiyoambukiza
2)
Tafiti kuhusu udhibiti wa ugonjwa wa
matende na mabusha
3)
Miaka 50 ya uhuru: Mchango wa Utafiti
katika sekta ya Afya
4)
Vita dhidi ya Malaria: Nini Kifanyike
5)
Mchango wa utafiti katika
kuboresha,  kurekebisha au kutunga sera
6)
Vipaumbele vya Taifa vya Utafiti
kuhusu ugonjwa wa Ukimwi kwa mwaka 2011/2012.


Malengo
ya Kongamano
Kongamano hili
linalenga kuwashirikisha watafiti, watunga sera na wadau wa afya duniani ili
kubadilishana uzoefu katika Nyanja mbalimbali za kisayansi.
Watafiti mbalimbali kutoka
katika nchi za Afrika zikiwemo Tanzania, Afrika ya Kusini, Senegal, Marekani na
Zambia wanatarajiwa kushiriki katika kongamano hilo ambapo mbalimbali zipatazo  zitajadiliwa.

Ni matarajio ya Taasisi
kuwa katika kipindi cha siku nne cha kongamano hilo, washiriki
wataweza
kufikia maazimio kuhusu hatua iliyofikiwa na Tanzania katika kutekeleza malengo
ya maendeleo ya milenia kuelekea mwaka 2015, na pia kuweza kupanga vipaumbele
vya utafiti wa ugonjwa wa ukimwi katika mwaka 2011-212.
Vilevile katika
harakati za kuhamasha watafiti waliobobea na wale wanaokua katika utafiti; NIMR
inatarajia kutoa Tuzo za Kisayansi nne
kwa mawaka huu wa 2012 kama ifuatavyo:
1.
Outstanding
Scientist of the Year Award 2012 (Tuzo ya Mwana Sayansi Bora wa mwaka) :
Tuzo
hii pia inatolewa kwa mara ya kwanza na NIMR ili kutambua kazi zinazofanywa
nawatafiti nchini. Inatolewa kwa mtafiti bora nchini ambaye kazi zake za
utafiti zimeweza kuleta mabadiliko katika masuala mbalimbali yakiwemo ya
uvumbuzi wa teknolojia au mifumo ya utoaji huduma katika sekta ya afya au
uvumbuzi ambao umechangia kuundwa au kurekebishwa kwa sera katika sekta ya afya
nchini.
2.
Mount
Kilimanjaro Scientific Award
Mwanzilishi
wa Tuzo hii ni Dakta Leonard Mboera , ambaye ni Mkurugenzi wa TEKNOHAMA-NIMR.
Tuzo hii inatolewa kwa mwanasayansi bora, ambaye ni chipukizi aliyewasilisha
vyema mada za kiutafiti katika kongamano hili la kisayansi.Tuzo hii inalenga  kuhamasiha wanasayansi chipukizi kushiriki
zaidi katika kazi za utafiti.

3.
Dr.
Maria Kamm Best Woman Scientist Award
Tuzo
hii inatolewa kwa mara ya kwanza mwaka huu na imeanzishwa rasmi na Dakta Mwele
Malecela ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR. Lengo la tuzo hii  kuenzi jitihaba za Mama Maria Kamm katika
kuhamasisha wanawake kushiriki katika Masomo ya sayansi wanapokuwa mashuleni,
jambo ambalo limesaidia kuongeza idadi ya watafiti wa Kisayansi nchini na hata
NIMR.
Mama
Maria Kamm alikuwa Mwalimu Mkuu maarufu wa Shule ya Sekondari wa Wasichana ya
Weruweru ambaye alibobea katika miaka ya 1970, kwa umahiri wake katika kazi na
kwa kuzingatia maadili halisi ya kazi ya ualimu.
Mama
kamm alikwa ni miongoni mwa walimu wachache kwa kipindi hicho waliopata Shahada
ya Ualimu katika Chuo Kikuu cha Notre Dame.
Tunamuenzi
Mama Maria Kamm kwa juhudi zake katika kuzalisha wanawake watafiti na viongozi katika
sekta mbalimbali jambo ambalo limechangia kuinua uwezo wa wanawake katika
kuongoza na kuleta maendeleo ya jamii.
4.
Professor
Wenceslaus Kilama Best Upcoming Award
Tuzo
hii inalenga kumuenzi aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa Kwanza wa NIMR katika miaka
ya themanini Professor Wenceslaus Kilana ambaye alikuwa mchapa kazi na
aliyependa kupima matokeo  halisi ya kazi
za wanasayansi sambamba na uwezo wa mwanasayansi katika kuvumbua mambo mapya
kupitia utafiti, na hasa kwa kwa wanasayansi chipukizi.
Tuzo
hizi zitakuwa zikitolewa kila mwaka katika kongamano hili la Kisayansi
Ndugu Wanahabari,
Napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha taasisi
mbalimbali za serikali na waandishi wa Habari wanaoviwakilisha vyombo vya
Habari vilivyopo mkoani Arusha kuhudhuria kongamano hili, ili kupata taarifa
mbalimbali za utafiti hatimaye kuweza kutoa taarifa hizo kwa Watanzania na
kukuza weledi wa jamii kuhusu mbinu za kuimarisha afya ya binadamu kupitia
utafiti. 

ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA


0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa