Na Mary Ayo,Arusha
WADAU wa Benki ya Maendeleo ya Afrika wanatarajia kukutana jijini Arusha May 26 mpaka June mosi ambapo kupitia mkutano huo wadau mbalimbali hasa wa mkoa wa Arusha wataweza kunufaika na Mkutamno huoi ikiwa ni pamoja na kupata mbinu za kujiunga katika mtandao wa benki hiyo.
Akizungumza na Vyombo vya habari Mjini Arusha Kamishna kutoka Wizara ya Fedha Bw Ngosha Maponya alisema kuwa kupitia mkutano huo wanannchi wa Tanzania wataweza kunufaika sana na mkutano huo kwa kuwa watapata fursa mbali mbali ndani ya mkutano huo Bw Maponya alieleza kuwa wanatarajia mkutano huo kuhudhiuriwa na watu 2000 hadi 3000 kutoka maeneo mbalimbali ambapo zaidi ni kuimarisha uchumi wa wadau w benki hiyo.
Alifafanua kuwa kupitia mkutano huo asilimia kubwa ya washiriki wataweza kupata faida mbalimbali ambapo faida kubwa ni kuimarisha na kujiamini katika masuala ya biashara hali ambayo nayo itachangia kwa kiwango kikubwa sana ongezeko la uchumi wan chi ya Tanzania .
“ndani ya mkutano huo fursa mbalimbali zitaweza kjuibuka ambapo kupitia fursa hizo zitasaidia sana katika kuimarisha uchumi wa nchi ya Tanzania na huku faida nyingine na watanzania kuweza kukutana na wadau mbalimbali wa benki hiyo ambao wanalenga kuimarisha uchumi”alisema Bw Maponya.
Mbali na kuimarika kwa shughuli za uchumi ambapo ni moja ya malengo ya Nchi ya Tanzania pia Mkutano huo utaweza kuimarisha Tanzania hususani mji wa Arusha ambapo kuna aina mbalimbali ya utalii wa ndani ambapo kupitia mkutano huo mji huo utaweza kujitangaza zaidi utalii wake.
Alifafanua kuwa wadau hao kupitia kwa wenyeji wataweza kushiriki katika mkutano huo huku biashara ndogondogo zikiwemo za utalii wa ndani nazo zikiendelea hali ambayo nayo itawanufaisha sana wafanyabaishara wa mkoa wa Arusha.
Awali Aliwataka Watanzania wote kuhakikisha kuwa wanashiriki katika mkutano huo ambao unalenga kuimarisha hata uchumi wa Watanzania kwa kiwango cha hali ya juu sana
0 comments:
Post a Comment