“Kesi ya kashfa haiwezi kufunguliwa na mtu mwingine isipokuwa yule aliyekashifiwa. Shauri la kashfa haliwezi kuwa na uwakilishi ndiyo maana ikitokea mlalamikaji katika kesi ya kashfa anafariki dunia, basi shauri lenyewe nalo huishia hapo kwa sababu haliwezi kurithiwa,”
Dk Burian aliyedaiwa kukashifiwa na Lema hakufungua kesi wala hakufika mahakamani kutoa ushahidi kuhusu madai hayo licha ya Jaji Rwakibarila kusisitiza umuhimu wa ushahidi wake kutokana na kutajwa na mashahidi wote 14 wa upande wa wadai walioitwa mbele yake.
Shilinde Ngalula
Mkuu wa Kituo cha Sheria na Haki za binadamu (LHRC),
Kanda ya Arusha,
Chanzo;http://mwananchi.co.tz
0 comments:
Post a Comment