Said Mwishehe, Arumeru
WANAFUNZI
wanaotoka kwenye kaya maskini nchini zaidi ya milioni mbili ni
miongoni mwa wafaidikaji wakuu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF)
imeelezwa.
Aidha wanafunzi hao wanapofika chuo kikuu hupata mkopo
kwa asilimia 100 ili kuwawezesha kukamilisha masomo yao kutokana na
familia zao kutokuwa na uwezo wa kutoa nyongeza.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa TASAF, Shedrack Mziray, kati ya
wafaidikaji wote Milioni5.19 wanafunzi pekee ni Milioni2.13 ambao ni
sawa na asilimia 41.
Mziray amesema kati ya wanafunzi 2,139,500
waliohudumiwa, wanafunzi wanawake walikuwa 1,074,445 na wanaume ni
10,65,055 ambao wote wana umri wa kati ya miaka 6 hadi 18.
Amesema mradi huo umetekelezwa katika Halmashauri 186 nchini ambapo pia wanawake ndio wanufaikaji wakuu zaidi ya wanaume.
"Katika
idadi hiyo ya wanufaikaji, wanawake ni 2,892,643 sawa na asilimia 55.7
na wanaume ni 2,302,962 ambao ni sawa na asilimia 44.3, hapa utaona
Wanawake ni wengi tofauti na wanaume,"amesema.
Aidha Mziray
amesema mfuko huo hivi sasa uko kwenye tathmini ya utekelezaji wake ili
kuweza kubaini wanufaikaji wanaotakiwa kuondolewa baada ya kufanikiwa
kupitia ruzuku ambayo wamekuwa wakipata kupitia TASAF.
" Moja ya
sera na masharti ya mfuko wa TASAF ni kuwanyanyua wahitaji kutoka hali
duni kwenda katika hali ambayo ataweza kujitegemea kiuchumi, hivyo hivi
sasa hadi Septemba 2024 tunatarajia kuondoa wanufaikaji 400,000 ambao
hali zao za maisha zimeimarika," amesema.
Kwa upande wake Sara
Mshiu ambaye ni Meneja Akiba na kupunguza umaskini wa kaya wa mfuko wa
TASAF anasema moja ya changamoto kubwa walizokabiliana nazo ni uwepo wa
kaya hewa ambazo hazistahili kupata msaada kupitia mfuko huo.
Hata
hivyo amesema baada ya kubaini hilo, mfuko ulitengeneza mfumo dhabiti
wa kubaini kaya hizo na umeweza kuziondoa kwa zaidi ya asilimia 90.
"
Changamoto kubwa ilikuwa ni kuingizwa kwa kaya hewa, na wakati mwingine
baadhi ya viongozi waliokuwa wakiratibu kuandikisha majina walishindwa
kuwaondoa kwa kuogopa hadi uchawi, lakini baada ya kutengenezwa mfumo
mzuri, wote waliondolewa,"amesema Sara.
Mfuko wa TASAF
ulianzishwa mwaka 2000 nchini ambapo hivi sasa inatekeleza awamu ya tatu
ya mradi huo ulioanza mwaka 2020 na kutarajiwa kutamatika Septemba
2025.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Shedrack Mziray
akizungumza na Wahariri pamoja na waandishi wa habari kuhusu Miradi
inayosimiwa na Mfuko huo ukiwemo wa kuziwezesha kiuchumi kaya masikini .
Wahariri na waandishi hao wapo Mkoani Arusha kwa ajili ya kutembelea
wanufaika wa Mfuko huo.
Mmoja
ya jengo la bweni la Shule ya Sekondari Oldonyowas lililojengwa na
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) baada ya Wananchi kuomba kujengewa
mabweni pamoja na shule hiyo
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Shedrack Mziray
akifafanua jambo kuhusu ujenzi wa shule ya Sekondari ya Oldonyowas
ambayo ujenzi wake umetokana na Mfuko huo.
Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Oldonyowas wakiwa makini kuzikiliza taarifa inayohusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ambavyo katika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya elimu mkoani Arusha.
Mwenyekiti wa Kata ya Oldonyowas katika Halmashauri ya Arusha Geofrey Ayo akizungumza wakati maofisa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wao Shedrack Mziray pamoja na waandishi wa habari walipotembelea shule ya Sekondari Oldonyowas iliyojengwa kwa fedha za Mfuko huo.
Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Oldonyowas wakiwa makini
kufuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF) hayuko pichani baada ya kutembelea shule hiyo iliyojengwa kwa
fedha za Mfuko huo.
Matukio mbalimbali katika picha baada ya waandishi, Wahariri na maofisa wa TASAF walipokuwa katika ziara ya kutembelea miradi na wanufaika wa Mfuko huo.
0 comments:
Post a Comment