Home » » WATUMISHI WATANO NCAA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA DOLA ZA KIMAREKANI 35,500

WATUMISHI WATANO NCAA WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUISABABISHIA SERIKALI HASARA YA DOLA ZA KIMAREKANI 35,500

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Na.Vero Ignatus Arusha.

Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro(NCAA])wamefikishwa mahakamani leo kwa kosa la kuisababishia hasara serikali na kusababisha hasara ya dola za Kimarekani 35,500.

Watuhumiwa waliofikishwa kizimbani na kukabilia na shitaka moja ni pamoja na Joseph Mtwala{36},John Mlambo{42},Mwahu Yunus {38},Mery Njau{38} na Catherini Edward {33}.

Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walisomewa shitaka moja na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa{TAKUKURU} ,Adamu Kilongozi akiwa na Hamidu Simbano na Richard Jacopiyo kuwa walitenda kosa hilo kati ya desemba 25 mwaka 2013 na juni 6 mwaka 2014.

Kilongozi alidai mahakamani hapo kuwa watuhumiwa hao wakiwa katika lango la Nabi Mkoani Mara na lango kuu la Loduare Mkoani Arusha watuhumiwa hao walisababishia serikali hasara ya fedha za Kimarekani kiasi hicho wakiwa watumishi wa NCAA.

Mwendesha mashitaka huyo alisoma shitaka hilo mbele ya Hakimu mkazi wa mahakama ya wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha,Bernad Nganga na kueleza kuwa walifanya kosa hilo huku wakijua ni kinyume na sheria.


Watuhumiwa wote walikana shitaka hilo na walipewa dhamana ya fedha taslimu shilingi milioni 7.9 au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo na taratibu za dhamana zilikuwa zikiendelea .

Mwendesha mashitaka wa TAKUKURU alisema kuwa ushahidi wa kesi hiyo umekamilika na aliiomba mahakama hiyo kupanga Tarehe ya kuanza usikilzwaji wa awali
Watuhumiwa wote watano wamepelekwa rumande kwakushindwa kukidhi masharti ya dhamani ,ambapo watasomewa hoja za  awali April 10 mwaka huu.




0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa