Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. Andrew W. Massawe akiweka saini kwenye kitabu cha
wageni mara baada ya kuwasili Wilaya ya Longido na kupokelewa na Katibu Tawala.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu NIDA (kushoto), akifuatiwa na Afisa Usajili Wilaya ya Longido
Ndg. Tarimo wakisikiliza taarifa ya mwenendo wa Usajili wananchi kwa Wilaya ya
Longodo iliyowasilishwa na Katibu Tawala Ndg. Toba Nguvila (Katikati). K kulia
ni Ndugu Alphonce Malibiche Kaimu Mkurugenzi Idara ya Uzalishaji.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu NIDA Ndg. Andrew W. Massawe (wa kwanza kushoto) akiwa
ameambatana na Katibu Tawala Wilaya ya Longido Ndg.Toba Nguvila wakiwa
wamewasili kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi za NIDA wilaya ya Longido na
kupokelewa na mkandarasi wa ujenzi ndugu Kim na maafisa wengine.
Muonekano
wa Ofisi ya Usajili Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Wilaya ya Longido
mkoani Arusha, ikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu (NIDA) Ndg. Andrew W. Massawe ametembelea na kukagua hatua za
ujenzi wa majengo ya ofisi katika Mkoa wa Arusha; na kukutana na viongozi mbalimbali
wa mkoa huo kujadili maendeleo ya zoezi la Usajili wananchi linaloendelea
nchini kote.
Ujenzi
wa Ofisi za NIDA unaoendelea katika Wilaya za Arusha, Arumeru na Longido ni
mradi wa mkopo wenye masharti nafuu unaofadhiliwa na Serikali ya Korea Kusini.
Akizungumza
na Katibu Tawala Wilaya ya Longido mara baada ya kukamilisha ukaguzi wa majengo
hayo; ndugu Massawe amesema majengo hayo yatawezesha NIDA kufanikisha malengo
ya Usajili kwa asilimia kubwa, pamoja na kurahisisha usafirishaji wa Data kwenda
makao makuu ya uzalishaji Vitambulisho kwakuwa majengo hayo yamejengwa kisasa
na yana miundombinu ya kuwezesha uzalishaji wenye kukidhi vigezo
vinavyohitajika kutokana na teknolojia inayotumika.
Wilaya
ya Longido Mkurugenzi huyo alipokelewa na Katibu Tawala Ndg. Toba Nguvila kwa niaba
ya Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye ameishukuru NIDA kwa hatua kubwa ya ujenzi wa
jengo la kisasa kwenye wilaya mpya ya Longido; ambalo si tu litasaidia
kuondosha uhaba wa Ofisi lakini kuwezesha Taasisi nyingine kama RITA na
Uhamiaji kupata ofisi zitakazowahudumia wananchi kwa ufanisi mkubwa zaidi
tofauti na hali ya sasa.
Kwa
mujibu wa Mkandarasi Kampuni ya KT –Korea; Ujenzi wa majengo hayo unatazamiwa
kumalizika mapema mwezi Mei mwaka huu; na kukabidhiwa NIDA kwa ajili ya kuanza
matumizi.
0 comments:
Post a Comment