Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Herry James
akisalimiana na baadhi ya viongozi wa UVCCM Mkoa wa Arusha mara baada
ya kuwasili Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Picha Na Mathias Canal
Na Mathias Canal, Arusha
Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa Ndg Herry James
amesifu ushirikiano wa wananchi Mkoani Arusha kwa kuunga mkono juhudi
za serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli katika kusimamia rasilimali za
Taifa.
Mwenyekiti
huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM ameeleza hayo Mara
baada ya kuwasilia Mkoani Arusha leo 10 Januari 2018 katika ziara yake
ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki
kampeni za kumnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Longido katika
uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Akizungumza
na Vijana wa Chama Cha Mapinduzi waliozuru kumlaki katika Mtaa wa
Tengeru, Wilaya ya Meru, Herry aliwasisitiza Vijana hao kuendeleza
mahusiano mazuri kwa Chama na serikali ili kuwa na jamii yenye nidhamu,
weledi na mtazamo chanya katika utendaji.
Alisema
pia mahusiano mazuri ndio msingi wa ushindi wa ngazi mbalimbali ikiwemo
uchaguzi mdogo wa udiwani uliomalizika hivi karibuni na CCM kuibuka
kidedea kwa zaidi ya asilimia 97%.
Aidha,
Herry amewafikishia vijana hao salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa kuwa amemuelekeza
kushiriki kampeni za Uchaguzi mdogo ambapo pamoja na mambo mengine Rais
Magufuli anatarajia matokeo ya ushindi wa kishindo katika chaguzi zote
za marudio nchini.
Aliongeza
kuwa katika kipindi kirefu Mkoa wa Arusha umekuwa na viongozi wasiokuwa
na maamuzi lakini kupitia serikali ya awamu ya Tano viongozi wengi
wamekuwa na maamuzi muhimu na mazuri kwa wakati sahihi huku akisifu
uwajibikaji wa Kamishna wa CCM Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa
huo Mhe Mrisho Gambo.
Sambamba
na hayo pia amewasihi Vijana wote nchini kusimamia kile wanachokiamini
kwa maslahi ya wengi na kuwa na maamuzi yakinifu kwa wakati sahihi.
0 comments:
Post a Comment