Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (AUWSA), Mhandisi Ruth
Koya wakipeana mikono na Mkandarasi-Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering
ya China, Chen Xianghua mara baada ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa
mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa Jiji la
Arusha.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (AUWSA), Mhandisi Ruth
Koya akisaini mkataba wa utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya
majisafi na usafi wa mazingira kwa Jiji la Arusha, kushoto ni Mkandarasi
kutoka Kampuni ya Jiangxi Geo-Engineering ya China, Chen Xianghua
wanaotekeleza mradi huo.
Sehemu
ya wageni waliohudhuria hafla ya kusaini mkataba wa utekelezaji wa
mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa Jiji la
Arusha.
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (AUWSA), Mhandisi Ruth
Koya (kushoto), Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha ambaye pia ni Mkuu wa
Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro (katikati) na Waziri wa Maji na
Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe katika hafla ya kusaini wa mkataba
wa utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma ya majisafi na usafi wa
mazingira kwa Jiji la Arusha.Waziri
wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza katika
hafla ya kusaini wa mkataba wa utekelezaji wa mradi wa kuboresha huduma
ya majisafi na usafi wa mazingira kwa Jiji la Arusha.
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Maji na
Umwagiliaji kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa
Mazingira Jijini Arusha (AUWSA), leo imeingia mikataba ya Dola za
Marekani 233,915,581 ambazo ni takribani Shilingi 514,614,278,200 za
Tanzania kumaliza kabisa tatizo la maji katika Jiji la Arusha na Wilaya
ya Hai, Mkoani Kilimanjaro.
Fedha
hizo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB) ambao wamechangia Dola za Marekani 210,962,581 na Serikali ya
Tanzania ikichangia Dola 22,953,000 ili kukamilisha mradi huo.
Kazi
zitakazotekelezwa ni uchimbaji wa visima virefu, ujenzi wa matenki,
ulazaji wa mabomba ya majisafi na majitaka, ujenzi wa mtambo wa kutibu
maji, ujenzi wa mabwawa mapya ya kutibu majitaka, ujenzi wa Makao Makuu
ya Mamlaka na Ofisi za Kanda pamoja na ununuzi wa vitendea kazi.
Kukamilika
kwa mradi huu kutawezesha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama
kwa wakazi wa Jiji la Arusha kwa asilimia 100 hadi mwaka 2030 na
kutapunguza kiasi cha maji yanayopotea kutoka asilimia 45 ya sasa mpaka
kufikia asilimia 20. Aidha, mradi utaongeza mtandao wa kuondoa majitaka
kwa asilimia 30. Mradi huu unategemea kuchochea ukuaji wa uchumi wa
viwanda na kuboresha huduma nyingine za kijamii zikiwemo Afya na Elimu.
Hali
ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Jijij la Arusha kwa sasa ni
asilimia 44, sawa na wastani wa lita milioni 40 kwa siku na mradi huu
unategemea kuongeza kiwango na kufikia lita milioni 200 kwa siku.
0 comments:
Post a Comment