Mkurugenzi
wa Shirika lisilo la kiserikali la Haki Elimu
nchini John Kalage akipanda mti katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii
iliyoambatana na upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya
sekondari ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na
wafanyakazi wa shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu jana (Habari Picha Na Pamela Mollel,Arusha)
Wafanyakazi
wa shirika la Haki Elimu nchini wakiongozwa na Mkurugenzi wao John Kalage wa
tatu kushoto, wakichimba shimo kwaajili ya kuhifadhi taka ngumu katika shule ya
Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii
Wafanyakazi
wa shirika la Haki Elimu nchini wakijiandaa kwenda kupaka rangi madarasa katika
shule ya Sekondari Mukulat katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii
Mkurugenzi wa Shirika lisilo la kiserikali la Haki Elimu nchini John Kalage akipongezwa na Mkuu wa shule hiyo Vitalis Nada mara baada ya kumaliza zoezi la upandaji miti katika shule hiyo jana
Mmoja
wa wazazi shuleni hapo akishiriki zoezi la umwagiliaji wa maua
katka maadhimisho ya huduma kwa jamii iliyoratibiwa na Shirika na Haki Elimu
Wafanyakazi
wa Haki Elimu wakiwa wananendelea na zoezi la upakaji rangi shule hapo jana
Aliyeshika
ndoo nyekundu ni Abraham Lazaro kutoka Idara ya Habari na uchechemuzi akiwa na
mfanyakazi mwenzake wakiendelea na zoezi la umwagiliaji katika shule ya sekondari ya mukulati iliyopo
Mkoani Arusha katika maadhmisho ya wiki ya huduma kwa jamii
Mwanafunzi
shuleni hapo akiwa amebeba ndoo kwaajili ya kubebea maji kwaajili ya shughuli ya
umwagiliaji shuleni hapo jana
Meneja Idara
ya Huduma, fedha na Utawala Daniel Luhamo akichimba shimo la kuhifadhia taka
ngumu shuleni hapo
Mfanyakazi
wa Haki Elimu Raphael akiendelee na shughuli ya upakaji rangi
Rose
Mwenda Mmoja wa wafanyakazi wa HakiElimu kutoka Idara ya Ushiriki na
Uwajibikaji wa jamii akipaka rangi bati katika shule ya Mukulat iliyopo Mkoani Arusha
Mwanafunzi
wa kidato cha nne shule ya Sekondari Mukulat
Stella Massawe akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa HakiElimu John Kalage,
zawadi iliyotengeneza katika klabu yao
ya wanafunzi ya Njoo Tuzungumze
Mkuu wa
Miradi HakiElimu - Boniventura Godfrey akibeba ndoo za kuchotea maji kwaajili
ya umwagiliaji
Baadhi ya
wazazi wakisalimia katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana
na uapandaji wa miti na tunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya
mukulati iliyopo Mkoani Arusha shughuli iliyohudhuriwa na wafanyakazi wa
shirika hilo ,wazazi na wadau wa elimu
Afisa Elimu
Taaluma Halmashauri ya Wilaya Arusha Vijijini ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa
Halmashauri akimkabidhi zawadi iliyotolewa na bodi ya
shule kwa Mkurugenzi wa Haki Elimu nchini John Kalage kwa kutambua umuhimu wa
elimu Nchini
Picha ya
pamoja
Na Pamela
Mollel,Arusha
Shirika lisilo
la kiserikali nchini Haki Elimu limetoa shilingi milioni ishirini ya kuanzishwa
kwa ujenzi wa kisima cha maji katika shule ya sekondari mukulat katika kijiji
cha lemanyata kata ya lemanyata wilaya ya arusha vijijini ili kuwaondolea adha
wanafunzi i wa shule hiyo wanaolazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia muda
mwingi kwakutafuta maji.
Akizungumza
katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii iliyoambatana na uapandaji wa
miti na utunzaji wa mazingira katika shule ya sekondari ya Mukulat Mkurugenzi
wa haki elimu nchini john kalaghe amesema shirika la haki elimu limeamua
kushirikiana na jamii katika kuondoa changamoto katka sekta ya elimu katika
shule hiyo ikiwamo tatitzo la maji pamoja na kuboresha mazingira kwa kupanda
miti pamoja na kukarabati majedarasa hayo kwa kupiga rangi.
Shirika hilo
la haki elimu kwa kupitia kwa mkurugenzi huyo wameahidi kutoa ufadhi kwa
kuwalipia karo wanafunzi wa shule ya sekondani ya mukulat watakaofanya vizuri kwa ufaulu wa daraja la
kwanza katika mtihani wa kidato cha nne unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni ili
kutoa hamasa kwa wanafunzi wengine kufanya vizuri katika mitihni hasa kwa mtoto
wa kike ambaye anaonekana yuko nyuma kwa mambo ya elimu hasa katika jamii ya
kifugaji.
Akizungumza
kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaa ya Arusha vijijini katika
maadhimisho ya wiki ya huduma kwa jamii ,afisa elimu wa wilaya hiyo B akari kimath
amelipongeza shirika la haki elimu kwa kuanzisha mradi wa maji katika shule
hiyo pamoja na upandaji wa miti na ukarabati wa madarasa na amesema miradi hiyo
itapunguza changamoto za elimu zinazozikabili shule za msingi na sekndari
wilayani humo na kuliomba shirika hilo kuendela na msaada huo katika shule
zilizoko pembezoni mwa wilaya ili kuwawezesha wanafunzi kupata elimu bora
Ameiomba
jamii kushirikiana na mashirika yasyoyakiserikali kupungumza changamoto yanaozikabili shule za msingi na sekondari na
kuitaka jamii kuhakikisha wanatunza miradi hiyo ili iweze kuwasaidia wanafunzi
walikuwa wanapata shida kwa usafuri umbali mrefu kutafuta maji.
Kwa upande
wake mkuu wa kitengo cha miradi shirika la haki elimu Boniventura Godfrey amesema kwa kutambua changamoto zinazoikabili
sekta ya elimu nchni tayari wameanzisha mpango maalumu wa kuzisaidia shule za
msingi na sekondari 127 katika wilaya
ishirini na mbili kwa kuwasaidia miradi ya maji,uwekaji wa umeme wa jua
,ukarabati wa madarsa,na upelekaji wa vifaa vya elimu ili kuwawezesha wanafunzi
kuapata elimu katika mzngira bora.
Awali wakizungumzi
miradi hiyo wanafunzi wa shule ya sekondari Mukulat Stella Massawe wamelishukuru shirika la haki
elimu kwa uboreshaji wa miundombinu katika shule hiyo kwa kuwa mradi huo wa
maji utawapungumzia changamoto iliyokuwa ikiwakabili kwa kusafuri umbali mrefu
kwa kutafuta maji pamoj na kutumia muda wa masomo hivyo ,kupungua kwa
changamoto hizo kutapunguza suala la utoro kwa wanafunzi.
0 comments:
Post a Comment