Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
1
Kaimu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Hifadhi Hati Bi. Rose Mdami akikagua
fomu ya Bwana Kitomari baada ya kukamilisha hatua ya kwanza ya usajili
Vitambulisho vya Taifa kabla ya kwenda kwenye hatua ya upigaji picha.
Hapa ni Kata ya Makiba kituo cha CCM Arumeru Arusha ambako zoezi hilo
linafanyika.
Hawa
ni Watendaji katika vitongoji viwili vya Kijiji cha Valeska wakiendelea
na zoezi la kuwahakiki wananchi wao na kuwathibitisha kuwa ni wakazi
halali wa eneo lao kabla ya kuwaidhinisha kupigwa picha na kuchukuliwa
alama za vidole wakati wa zoezi la Usajili linaloendelea Wilayani
Arumeru.
Huu
ni muonekano wa nje ya jengo ambako usajili wa Vitambulisho vya Taifa
unaendelea Kata yaMakiba kijiji cha Valeska. Baadhi ya wananchi wakiwa
wanabadilishana mawazo huku wakisubiri kupatiwa huduma.
Afisa
Usajili Wilaya ya Arumeru ndugu Edward Bujune akitoa maelezo kwa
wananchi kuhusu umuhimu na faida za Vitambulisho vya Taifa wakati zoezi
la kuwasajili wananchi wa Wilaya ya Arumeru likiendelea.
Meneja
Mifumo ya Komputa ndugu Mohamed Mashaka akirekebisha moja ya Kamera ili
iweze kufanya kazi kwa ufanisi zaidi wakati wa ziara ya kukagua
utekelezaji wa zoezi la Usajili Wilayani Arumeru.
Meneja
Uthibiti na Usambazaji ndugu George Mwandezi aliyeshika Kitambulisho
akitoa elimu kwa wananchi kuhusu ubora wa Vitambulisho vya Taifa wakati
wakiendelea na zoezi la Usajili Kata ya Makiba wakati viongozi hao
walipofanya ziara kukagua maendeleo ya zoezi linaloendelea sasa katika
Kata hiyo.
Mtendaji
katika Kijiji cha Valeska Kata ya Makiba akihakiki fomu za wananchi
kabla ya kuingia kwenye chumba cha uchukuaji alama za vidole, picha na
saini ya kielektroniki. Fomu hizo zimekuwa zikusanywa na kupitiwa iwapo
zimekamilika kujazwa vipengele vyote 72 vinavyohitajika
Hawa
ni baadhi tu ya wananchi katika kijiji cha Valeska wakiwa kwenye foleni
ya picha na uchukuaji alama za kibaiolojia wakati zoezi la Usajili
likiendelea kijini hapo.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida, wananchi katika Wilaya ya Arumeru Kata ya
Makiba kijiji cha Valeska mkoani Arusha; wameonyesha kuelewa umuhimu wa
Vitambulisho vya Taifa kiasi cha kujiwekea mkakati wa kuhakikisha
nishati ya umeme muda wote inakuwepo ili zoezi la Usajili linaloendelea
kutosimama.
Pengine
hii ni tofauti na mazoea ya siku zote katika uendeshaji wa zoezi la
Usajili na Utambuzi wa Watu kwa maeneo ambayo zoezi kama hilo limewahi
kufanyika kiasi cha kuamsha morali zaidi kwa watumishi kutokana na
mwamko mkubwa wa wananchi kushiriki zoezi hilo.
Akizungumza
kwa niaba ya wananchi wa Kata hiyo; mtendaji wa Kata hiyo amesema wao
kama Kata wamehamasisha wananchi kujitokeza kusajiliwa na kutokana na
ushirikiano mkubwa ulioonyeshwa na wananchi wana imani Kata yao
watakamilisha zoezi la Usajili ndani ya muda uliopangwa.
“Kama
unavyoona hapa wananchi ndo wamekwenda wenyewe kutafuta genereta baada
ya umeme kukatika na hawajashurutishwa na mtu… wamekusanyana na ghafla
tunashtukia wanafunga genereta wakati tukiwa bado tunatafakari namna ya
kufanya na wapi pa kupata huduma hiyo. Hii kwangu siyo kawaida kuona
wananchi wakijituma hivi kwenye zoezi la kitaifa. Wananchi wana mwamko
na shauku kubwa ya kuwa na Vitambulisho vya Taifa” alisema
Zoezi
la kuwasajili wananchi katika Mkoa wa Arusha limeanza kwa kasi kubwa na
katika Wilaya ya Arumeru zoezi hilo linaendelea katika Kata za Makiba,
Maroroni na Kikwe. Usajili huu unahusisha wananchi wote wenye umri wa
miaka 18 na kuendelea na unafanyikia kwenye vituo vya Usajili
vilivyoanishwa na NIDA kwa kushirikiana na Uongozi wa Wilaya ya Arumeru.
0 comments:
Post a Comment