Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wanawake
wa halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru wametakiwa kutumia jukwaa la
uwezeshaji wanawake kiuchumi kama chachu ya maendeleo yao na wanawake
wote ndani na nje ya halmashauri hiyo kwa kukaa pamoja ili kujengeana
uwezo na kushirikisha fursa za maendeleo.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake Halmashauri ya Arusha Katibu
Tawala wilaya ya Arumeru Timoth Mzava kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya
Arumeru amesema kuwa lengo la serikali kuanzisha majukwaa hayo ni
kuwakutanisha wanawake pamoja kutumia fursa ili kuchochea maendeleo ya
wanawake kiuchumi kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa na kutoa wito
kuwa majukwaa hayo yatumike kwa lengo lililokusudiwa.
Amesema
kuwa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi ni nyenzo muhimu kwa
maendeleo ya taifa hili hivyo msiishie kuunda majukwaa tu badala yake
mkatumie majukwaa haya kukabiliana na changamoto za kijamii, kiuchumi
kwa kutumia fursa zilizopo katika maeneo yenu na zile zinazotolewa na
serikali.
Aidha
amewataka wanawake hao licha ya Jukwaa hilo kujikita kwenye masuala ya
kiuchumi lakini pia kutumia majukwaa hayo kusimamia malezi bora ya
watoto, kupambana na mila na desturi potofu zinzomdhalilisha mtoto wa
kike pamoja na kujikita kusimamia maadili ya vijana wetu kwa maendeleo
ya taifa letu.
"Jukwaa
hili lisiishie kulianzisha tuu nendeni mbali zaidi tumieni Jukwaa hili
kwa kuitumikia jamii yetu kwa kusimamia malezi bora hasa maadili ya
vijana wetu, malezi ya watoto na familia kwa maendeleleo ya taifa letu"
amesisitiza
Jukwaa
hilo la halmashauri ya Arusha limekutanisha jumla ya majukwaa 27 kutoka
kata zote 27 za halmashauri ya Arusha na kuwakilishwa na wajumbe watano
kutoka kila kata na kufanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wa Jukwaa la
wanawake ngazi ya halmashauri.
Katika
uchaguzi huo jumla ya viongozi 7 walichaguliwa kwa kupigiwa kura na
mmoja aliteuliwa, hata hivyo Anna Msuya amechaguliwa kuwa
Mwenyekiti,Batuli Juma Makamu Mwenyekiti, Katibu ni Grace Seneu Mollel,
Katibu msaidizi Nosimu Kornelo, Mweka Hazina Asha Said na mjube wa
kuchaguliwa Chiku Mohamed na mjumbe mmoja wa kuteuliwa mwakilishi
walemavu ndugu Jacline Leonard na kupata jumla ya wajumbe 8 amabo
watawakilisha Jukwaa hilo ngazi ya mkoa.
Akizungumza
baada ya kuchaguliwa Mwenyekiti Ana Msuya amewataka wanawake wote
kuweka pembeni tofauti zao ikiwemo za kidini, kisiasa hata kiuchumi ili
kukabiliana na changamoto nyingi zinazowakabili wanawake wa halmashauri
ya Arusha.
"Tunaposimama
kwenye Jukwaa yatupasa kumuweka mwanamke kwanza, mwanamke ndio kila
kitu, ili kupambana na changamoto zinazotukabili tunaweka mbali tofauti
zetu pembeni kwa maendeleo yetu na taifa letu" amesema Mwenyekiti huyo.
Aidha
amewashukuru kwa kumuamini na kumchagua kuwaongoza na kuwaomba
kufanyakazi kwa pamoja kama timu na kusisitiza kuwa hata wale ambao
hawakuchaguliwa wanathamani sawa na wanawake wote waliochaguliwa hivyo
amewataka kutoa ushirikiano kwa viongozi waliochaguliwa.
Kabla
ya uzinduzi wa Jukwaa hilo, wanawake hao walipewa mafunzo ya
ujasiriamali na namna ya kutambua na kutumia fursa mbalimbali, majukumu
ya Jukwaa la wanawake kuanzia ngazi ya kata, wilaya, mkoa mpaka taifa
pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto.
Picha za matukio ya siku hiyo.
0 comments:
Post a Comment