Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Taasisi
ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewakaribisha wabunge wa
Chadema, Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru
Mashariki) kuwasilisha ushahidi wao kuhusu tuhuma za rushwa kwa madiwani
waliokihama chama hicho hivi karibuni.
Mkurugenzi
Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola amesema kuwa ofisi hiyo inawasubiri
wabunge hao kuwasilisha ushahidi wao ili waufanyie kazi kwa mujibu wa
sheria na taratibu.
“Bado
hawajatuletea ushahidi wowote lakini tunasubiri watuletee. Hakuna
shida, maadam wamesema hivyo, tunawakaribisha,” Mlowola anakaririwa na
Mwananchi.
Nassari
na Lema walieleza kuwa wanao ushahidi wa picha na video kuwa madiwani
wa Arusha ambao walihama chama hicho hivi karibuni na kujiunga na CCM,
waliotangazwa wakati wa tukio la Rais John Magufuli kutunuku kamisheni
kwa maafisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) mkoani humo walipewa rushwa.
Hata
hivyo, Madiwani hao walikana tuhuma za Nassari na Lema na kusisitiza
kuwa walikihama chama hicho kutokana na kuvutiwa na utendaji wa Rais
Magufuli. Waliwataka wabunge hao kuweka hadharani ushahidi walionao.
0 comments:
Post a Comment