Arusha
Home » » NSSF ARUSHA KUWASHTAKI WAAJIRI 126 KWA KOSA LA KUTOWASILISHA MICHANGO YA WAAJIRIWA INAYOFIKIA SHILINGI BILIONI

NSSF ARUSHA KUWASHTAKI WAAJIRI 126 KWA KOSA LA KUTOWASILISHA MICHANGO YA WAAJIRIWA INAYOFIKIA SHILINGI BILIONI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

 Meneja kiongozi wa NSSF mkoa wa Arusha katikati Dr. Frank Maduga akizungumza na waandishi wa habari juu ya kuwapeleka waajiri 126 mahakamani kwa kosa la kutowasilisha michango ya waajiriwa inayofikia kiasi cha shilingi bilioni moja nukta tano kwa kipindi cha miezi sita sasa. 

NA: ANDREA NGOBOLE, PMT

Jumla ya Kampuni 126 zinazodaiwa kiasi cha shilingi bilioni moja pointi tano zinatarajiwa kufikishwa mahakamani wiki ijayo na shirika la Taifa la hifadhi ya jamii NSSF mkoani Arusha kwa kosa la kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mapema jana meneja kiongozi wa NSSF mkoani Arusha Dr. Frank Maduga amesema kuwa makampuni hayo yamegawanyika kati ya waajiri wakubwa 14 wanaolipia kiasi cha shilingi milioni 50 na kuendelea, wajiri wa kati 69 wanaolipia milioni 5 hadi 49.9 na wale waajiri wadogo 53 wanaolipia kiasi cha shilingi elfu ishirini hadi milioni 4.9 kwa mwezi ambapo jumla ya michango yao inafikia Zaidi ya bilioni moja nukta tano mpaka sasa.

“Waajiri wakubwa wote wamekwisha pelekewa onyo la Mwisho na sasa taratibu za kimahakama zinaendelea hivyo kuanzia jumatatu ya tarehe 2 october 2017 mtawajua ni waajiri gani wameshindwa kutekeleza wajibu wao na kwa kiasi gani wanadaiwa kila mmoja wao” alisema dokta Maduga


Amesema kuwa Mashitaka yatakayokuwa yakiwakabali waajiri hao ni kutowasilisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati na kwa muda unaozidi miezi sita, kitendo hicho kimekuwa na madhara makubwa kwa wafanyakazi na wategemezi wao kwa kukosa huduma za matibabu , fao la uzazi na pia kuna baadhi ya wanachama taarifa zao za kumbukumbu hazioneshi fedha yoyote katika muda ule ambao michango haijawasilishwa na kusababisha taharuki na msongo wa mawazo kwa wafanyakazi husika.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa