Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katika
hali ambayo haikutarajiwa, Diwani wa Kata ya Kimandolu Jiji la Arusha
(Chadema), Mchungaji Rayson Ngowi akiongozwa na Katibu wa Itikadi na
Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ametangaza kumuunga mkono Rais John
Magufuli na kwa kuachia nafasi yake.
Alifanya
hivyo jana mbele Rais Magufuli wakati madiwani 10 wa Chadema
waliojiuzulu nafasi zao kwa nyakati tofauti kwenye halmashauri tatu za
Arusha na kujiunga na CCM walipoitwa wakati Rais alipokuwa akihutubia
baada ya kutunuku kamisheni kwa maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ) kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Hatua hiyo inafanya jiji la Arusha linaloongozwa na Chadema kupoteza kata mbili.
Madiwani wengine waliojitambulisha mbele ya Rais Magufuli ni wale waliojiuzulu katika halmashauri za Meru na Arusha Vijijini.
Mchungaji
Ngowi ndiye aliyekuwa wa kwanza kupanda jukwaani na kuanza kumwagia
sifa Rais Magufuli, “Mwanzoni nilikuwa sikuelewi lakini sasa nakuelewa
sana. Nataka Watanzania wote wakuunge mkono. Tunaona jitihada zako za
kuifanya Tanzania kuwa nchi ya asali na maziwa. Tuko pamoja na nashukuru
sana kwa kunipokea.”
Mwingine
aliyepanda jukwaani ni aliyekuwa Diwani wa Muriet, Credo Kifukwe ambaye
alisema, “Nimeamua kumuunga mkono Magufuli kutokana na kazi nzuri
alizofanya na kila mwenye akili timamu anaona.
Huko tulikokuwa ilikuwa mambo ya pingapinga hawataki kuona mazuri yanayoendelea, nimeamua kurudi CCM hapa kazi tu.”
Baadaye
Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM alisema, “Hawa wananchi
wanataka maendeleo kuliko majina ya vyama na maendeleo hayajali wewe ni
CCM , Chadema au CUF.”
Hata
hivyo, alionyeshwa kushangazwa na madiwani hao kuacha haki zao zikiwamo
masilahi mengine na kuamua kujizulu nafasi zao na kuwakaribisha CCM.
Pia, aliutaka uongozi wa CCM kuwapitisha madiwani hao kuwania tena nafasi hizo ili wakashindane na vyama vingine.
0 comments:
Post a Comment