Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Waziri
Lukuvi pamoja na viongozi wa mkoa wa Arusha wakifanya ukaguzi wa eneo
la Ekari mia moja (100) lililopimwa viwanja kwa ajili ya utatuzi wa
viwanja mbadala kwa Halmashauri ya jiji la Arusha.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi Mkuu wa
Mkoa Arusha Mrisho Gambo na Mkuu wa Wilaya Arusha Gabriel Fabian
wakiteta jambo wakati wa Uzinduzi wa Safari City.
Na. Hassan Mabuye
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amezindua
ujenzi wa Mji wa Safari pamoja na kuwapa hati wakazi 100 wa mji wa
Arusha.
Safari City ni mji wa kisasa uliopangwa vizuri kwa kufuata sheria na kanuni za mipango miji uliopo Jijini Arusha.Eneo hili limepangwa viwanja vya nyumba za makazi, ofisi, biashara, hoteli, shule na viwanda vidogo vidogo.
Viwanja hivi vina huduma zote muhimu kama vile miundombinu ya maji, umeme, barabara na mfumo wa maji taka.Mauzo ya viwanja hivi yanakwenda sambamba na mauzo ya nyumba za mfano ambapo viwanja vya makazi vinaanzia Tsh 7M na kuendelea.
Katika
ziara hii Waziri Lukuvi alipokea taarifa ya ufutwaji wa mashamba kumi
na mbili (12) yaliyoko Halmashauri ya Meru kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mrisho Gambo.
Baada
ya kupokea taarifa hiyo Mhe. Lukuvi alitembelea eneo la Ekari mia moja
(100) lililopimwa viwanja kwa ajili ya utatuzi wa viwanja mbadala kwa
Halmashauri ya jiji la Arusha.
0 comments:
Post a Comment