Mkuu wa Polisi Jamii mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Shabani Shabani
akitoa ufafanuzi juu ya sheria ndogo ndogo zinazoweza kumbana mtu
atakayekaidi kulipa michango ya ulinzi shirikishi katika eneo lake
(Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi)
Mmoja wa wananchi wa kata ya Moivaro halmashauri ya jiji la Arusha ambao
walihudhuria mkutano juu ya ulinzi shirikishi akiuliza swali na pembeni
yake ni mkuu wa Polisi Jamii mkoa wa Arusha Mkaguzi wa Polisi Shabani
Shabani akimsikiliza kwa makini (Picha na Rashid Nchimbi wa Jeshi la
Polisi Arusha)
Diwani wa kata ya Moivaro Bw. Rick Moiro akichangia jambo katika mkutano
uliokuwa unazungumzia juu ya ulinzi shirikishi katika kata yake (Picha
na Rashid Nchimbi wa Jeshi Polisi Arusha)
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Viongozi
wa kata na mitaa wametakiwa kutoumiza vichwa vyao na kuvutana mashati
na wananchi watakaokaidi kutoa michango katika masuala ya ulinzi na
badala yake wanatakiwa wawabane kwa kutumia sheria.
Akizungumza
jana katika mkutano uliofanyika mtaa wa Moshono Kaskazini kata ya
Moivaro tarafa ya Suye halmashauri ya jiji la Arusha, Mkuu wa Polisi
Jamii mkoa wa Arusha, Mkaguzi wa Polisi Shabani Shabani aliwaambia
viongozi pamoja na wananchi kuwa wanaweza kutunga sheria ndogo ndogo
kupitia sheria ya serikali za mitaa ya mwaka 2000.
“Hakuna
haja ya kuumiza kichwa bali viongozi mnapaswa kutumia kifungu namba 163
na 164 katika kitabu hicho wamezungumzia namna ya kutunga sheria ndogo
ndogo kulingana na mahitaji ya eneo lenu”
“Lakini
pia kifungu namba 167 kinazungumzia adhabu zinazoweza kutolewa kwa mtu
yeyote ambaye hatashiriki au atakayeshawishi kukwamisha masuala ya
ulinzi atatozwa faini ya Shilingi 50,000”. Alifafanua Mkaguzi huyo wa
Polisi Shabani Shabani.
Alisema
pia mbali na kitabu hicho cha sheria pia katika ibara ya 27 na 28 za
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zinazungumzia wajibu wa kila
mtanzania juu ya ulinzi wa mali za umma pamoja na kulilinda Taifa hivyo
aliwataka viongozi hao wafanye kazi zao kwa kujiamini na wafahamu kwamba
sheria juu ya hilo zipo wazi.
Alizidi
kuhamasisha viongozi hao kufufua kikundi cha ulinzi shirikishi ambacho
kinaonekana kusimama katika uteketezaji wa majukumu yake, na kutoa
mifano ya baadhi ya kata zilizopo halmashauri ya jiji la Arusha ambazo
zimepiga hatua kubwa katika kuimarisha vikundi hivyo vya ulinzi
shirikishi ambapo wana sare pamoja na silaha za moto na kuongeza kwamba
hali hiyo inatokana na hamasa ya wananchi wenyewe.
Alisema
vikundi hivyo vina faida kubwa katika suala zima la kuimarisha ulinzi
hasa ikizingatiwa kwamba askari wa Jeshi la Polisi wao pekee
hawatoshelezi kusambaa kila mitaa kwa mara moja kutokana na idadi yao
kuwa ndogo kauli ambayo iliungwa mkono na Mwenyekiti wa mtaa huo Bi.
Janeth Jonas.
Akichangia
wazo katika mkutano huo Diwani wa kata ya Moivo Bw. Rick Moiro alisema
pamoja na utaratibu wa kuwatambua na kuwabainisha wahalifu kwa njia za
siri kuendelea katika kata hiyo, lakini akasema ni vyema Jeshi hilo
likaanza kuwakamata wahalifu wanaojulikana badala ya kusubiri mpaka
orodha ya wahalifu wengi ipatikane.
Akijibu
malalamiko ya wananchi hao waliohudhuria kikao hicho juu ya baadhi ya
askari wa vikundi shirikishi hao kutoonekana mitaani wakati wa usiku kwa
madai kwamba huwa wanakwenda kulala, Mtendaji wa Kata hiyo Bw. Goodluck
Anderson alisema kwamba kwa sasa wananchi waondoe hofu na kuahidi
kulisimamia jambo hilo kwa ukaribu zaidi ili kuweza kubaini ukweli wa
malalamiko hayo.
0 comments:
Post a Comment