Imeandikwa na John Mhala,Arusha
MWILI wa bilionea wa Arusha, Faustine Mrema (65), atazikwa katika
shamba lake kubwa la ekari 80 lililopo wilayani Arumeru Mkoani Arusha
nyuma ya hoteli yake ya kifahari ya Ngurdoto iliyoko katika wilaya hiyo
Mrema aliyekuwa anamiliki hoteli za kifahari ikiwemo yenye hadhi ya
Nyota Tano ya Ngurdoto jijini hapa, unatarajiwa kuwasili jijini Arusha
leo mchana ukitokea Johannesburg, Afrika Kusini alikofikwa na mauti.
Kwa mujibu wa taarifa ya familia ya Mrema aliyekuwa pia mmilikiwa
hoteli za Impala ya Moshi na Arusha, Naura Springs ya Arusha na kampuni
kadhaa za utalii, nyumba na magari ya kukodisha, mwili wa bilionea huyo
utazikwa Jumatano ijayo nyuma ya hoteli yake ya Ngurdoto iliyopo Usa
River, wilayani Arumeru. Taarifa hiyo ilisema kuwa mwili wa Mrema
unatarajiwa kuwasili leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Kilimanjaro (KIA) majira ya saa 7 mchana.
Baada ya kuwasili, mwili huo utapelekwa moja kwa moja katika chumba
cha kuhifadhia maiti cha Hospital ya Rufaa ya Seliani inayomilikiwa na
Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) jijini Arusha. Taarifa
hiyo imesema Jumanne mwili huo utapelekwa nyumbani kwake eneo la
Uzunguni kwa ajili ya ibada .
CHANZO HABARI LEO
0 comments:
Post a Comment