Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akisalimiana na waendesha boda boda, eneo la kwa kwamromboo waliohuduriia kwenye uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Polisi
Baadhi wa wananchi waliohudhuria kushuhudia uwekaji wa jiwe la Msingi kwenye Kituo cha Polisi Muriet.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (kwanza kushoto) akiweka Jiwe la Msingi kwenye Ujenzi wa Kituo cha Polisi Muriet.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiwa na wafadhili Mr. Haroun, Mrs Haroun pamoja na Sailesh Pandit baada ya uwekaji wa Jiwe la Msingi.
Mke
wa Mfadhi Mrs Haroun akivishwa vazi la
Kimasai na wakazi wa eneo hilo kama shukrani yao kwa kujengewa Kituo cha
Polisi.
Nteghenjwa
Hosseah, Arusha
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo ameweka Jiwe
la Msingi kwenye Kituo cha Polisi Kata ya Muriet wakati wa ziara ya Kikazi
Jijini hapa yenye lengo la kukagua shughuli za maendeleo pamoja na kutatua kero
za wananchi.
Akiweka jiwe la Msingi Mhe. Gambo amesema kwa muda mrefu
alikua anakerwa na uhalifu uliokithiri katika eneo hilo na hali hiyo kumsukuma
yeye kutafuta mfadhili kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa kituo cha Polisi kitakachosaidia
kudhibiti masuala ya Uhalifu.
Aliongeza kuwa baada ya
kumpata mfadhili huyo alimlete eneo la ujenzi ambapo pia wahalifu walimuibia
Simu yake mbele ya viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndipo na mfadhili
alipopata ari ya kuanza ujenzi huu haraka iwezekanavyo.
“Haiwezekani mtu anaiba
mbele ya Kamanda wa Polisi hakika hii ilituthibitishia kwamba uhalifu katika
eneo hili umekithiri na kwa sababu hakunha Kituo cha Polisi wahalifu wanapata
mwanya wa kufanya kazi hii isiyo halali kwa ujasiri zaidi” Alisema Gambo.
Akizungumza wakati wa
hafla hiyo Mfadhili ambaye ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Lodhia Ndg. Haruni alisema amejitolea sehemu
ya mali zake ili kuwasaidia Watanzania wenzake wanaoteseka na tabia za uhalifu
zinazorudisha nyuma maendeleo
Ujenzi wa Kituo hicho
utakaogharimu zaidia ya Tsh Mil 200 utakamilika mnamo mwezi Juni 2017.
0 comments:
Post a Comment