Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro mara baada ya kutembelea eneo hilo kujionea changamoto za
kimazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Baraza la wafugaji (hawapo
pichani) katika Wilaya ya Ngorongoro. Wafugaji hao walimweleza Waziri kilio cha
muda mrefu cha mradi wa Josho Wilayani hapo, Waziri Makamba ameutaka uongozi wa
Mamlaka ya Ngorongoro na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
kuleta ufumbuzi mapema.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano
na Mazingira Mh. January Makamba akizungumza na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi
ya Ngorongoro mara baada ya kutembelea eneo hilo kujionea changamoto za
kimazingira.
Na
Lulu Mussa
Ngorongoro
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais mwenye dhamana ya usimamizi wa Mazingira nchini
Mhe. January Makamba amesema kuwa ni lazima hatua za haraka zichukuliwe ili
kudhibiti mimea inayohatarisha uoto wa asili katika Mamlaka ya Ngorongoro.
Katika
kutatua changamoto hii, Waziri Makamba ameagiza kuundwa kwa jopo la wataalamu
kutoka Tume ya Sayansi na Tecknolojia,
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, Hifadhi za Taifa
za Tanzania, Wizara ya Kilimo na Mifugo na Mamlaka ya Ngorongoro ndani ya miezi
sita kufanyika kwa utafiti wa kina wa kisayansi wa kubaini mbinu mpya ya
kupambana na mimea hiyo vamizi inayotawala mimea inayotumiwa na wanyama.
Akizungumza katika kikao kilichojumisha Wahifadhi wa
Mamlaka ya Ngorongoro na Wajumbe wa Baraza la wafugaji, Waziri Makamba amesikitishwa
na kitendo cha Uongozi wa Mamlaka ya Ngorongoro kushindwa kuandaa mpango kabambe wa usimamizi wa hifadhi baada ya ule
wa awali kuisha muda wake. Waziri Makamba ameuagiza uongozi wa Ngorongoro kuandaa
mpango huo mapema na kuwa shirikishi. " Mpango mtakoandaa hakikisheni kuwa
unakuwa shirikishi kwa jamii inayozunguka na wadau na Taasisi muhimu likiwemo
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC).
Waziri
Makamba pia ameagiza kufanyika kwa ukaguzi wa kimkakati wa Mazingira utakaojumuisha
Wilaya nzima ya Ngorongoro na kuitaka Mamlaka ya Ngorongoro kushirikiana na
Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kutekeleza wajibu huo
mapema. Ukaguzi huo wa kimkakati wa kimazingira kwa Wilaya hiyo unatazamiwa kutoa mtazamo wa hali
ya mazingira kwa miaka hamsini ijayo.
Aidha,
Waziri Makamba ameagiza kufanyika kwa Tathmini ya Athari kwa Mazingira ama Ukaguzi wa Mazingira katika Hotel zote
zilizopo eneo la hilo na kulitaka Baraza la Taifa la Hofadhi na Usimamizi wa
Mazingira (NEMC) kupita siku ya Alhamisi tarehe 30/03/2016 kuwaandikia adhabu na
kuwatoza faini wahusika wote ambao hawana vyeti hivyo. "Haiwezekani toka
mwaka 2004 Sheria ipo na mpaka leo watu wanaendea na mchakato, hii
haikubaliki!" Alisisitiza Makamba.
Katika
hatua nyingine Waziri Makamba ametoa miezi sita kwa wamiliki wa Hotel zilizopo
katika Mamlaka ya Ngorongoro kuwekeza katika mfumo mpya wa kuvuta maji kutoka Mto
Lukusale na kusitisha mfumo wa sasa wa kutoa maji kwenye creator. Pia Makamba ameutaka ungozi wa Mamlaka ya Ngorongoro ndani
ya miezi sita kuandaa ramani itakayoonyesha mito na vijito vyote vilivyopo
ndani ya hifadhi hiyo.
Waziri
Makamba ametoa maagizo hayo leo juu ya
namna bora ya kutumia rasilimali ya "creater" kwa ajili ya
utalii na Uhifadhi wa Mazingira, ikiwa
ni pamoja na utekelezaji wa zuio la mifugo ndani ya crater. Ziara maalumu na mahsusi ya kukagua
utekelezaji na uzingatiaji wa Sheria ya Mazingira inayofanywa na Waziri Makamba
hii leo imefika Wilayani Ngorongoro.
0 comments:
Post a Comment