Home » » TIGO YAENDELEA KUIMARISHA MTANDAO WA 4G INTANETI KANDA YA KASKAZINI

TIGO YAENDELEA KUIMARISHA MTANDAO WA 4G INTANETI KANDA YA KASKAZINI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Habari mdau tafadhali pokea codes,
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata (kulia) akionyesha laini ya 4G internet zitakazotumika kwenye mashindano ya Killi Marathon yaliyodhaminiwa na Kampuni hiyo.Kushoto ni Meneja Mauzo wa Tigo Moses Busee.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Tigo kanda ya Kaskazini George Lugata (kulia) akifurahi jambo na 
Meneja Mauzo wa Tigo Moses Busee mara  baada ya kuonyesha laini ya 4G intaneti
zitakazotumika kwenye mashindano ya Killi Marathon yaliyodhaminiwa na Kampuni hiyo.


KAMPUNI  ya  simu  za  mkononi  ya  Tigo  imeendelea  kuboresha huduma  ya  mtandao   wake wa wenye  kasi  kubwa  wa   4G  kanda  wa  kaskazini  mwa  Tanzania  hatua  inayolenga kuwarahisishia   wateja  wake  wa  maeneo  hayo  na  wageni 
kutoka  mataifa  mbali  mbali   wakiwemo  watakaoshiriki  katika  mashindano  ya  kimataifa  ya  Kilimanjaro  Marathoni   yanayotarajiwa  kufanyika mwishoni  mwa  mwezi  February  katika  mji    wa  Moshi.

Mkurugenzi   wa  mawasiliano  wa  kampuni  hiyo  Bw  George  Lugata  amesema  katika  kuhakikisha kuwa  lengo  hilo  linafikiwa   kampuni  imeanza  kuongeza  minara  ya  mawasiliano    ya  mtandao  wa 4G maradufu    na  maeneo  mengi   kwa  sasa  wateja    wao  wameendelea   kupata    huduma  hiyo  hiyo


"Kama  mnavyojua  kampuni  ya  Tigo  ndio  wadhamini  wakuu  wa  mbio  hizo  kwa  upande  wa kilomita 21  na  kama  mnavyojua  mashindano  haya  yanawaleta  pamoja  watu  kutoka  mataifa  mbali mbali  ambao  kwao  wanatumia  mitandao  yenye kasi  kubwa  sasa  tunataka  wasipate  shida  na wajisikie  wako  nyumbani  kwao    na  waweze  kutuma  picha  na  video  kwa  urahisi'Alisema  Bw, Geoge Lugatamkurugenzi  wa  mawasiliano  Tigo   kanda  ya  kaskazini

Baadhiya  wateja  wanaotumia  mtandao  wa  huo  wa  4G  ambao  una  kasi  kubwa  wamesema umewarahisishia  kazi  zao  na  kuwaokolea  muda  na  gharama  za  kusubiri  wakati   wanapohitaji  kupakua na  kutuma  picha  na  video   na  wameipongeza  Tigo   kwa  kuboresha huduma  na kuwa karibu  na  wateja  wake
Kimsingi  ukitumia  Mtandao  wenye  kasikubwa  unaokoa  gharama  na  muda  unaotumia kusubiri ukiwa  na mitandao  mingine , mfano  mimi  ninapenda sana  kupakua na kupakia  picha  na video   na  nilivyoanza  kutumia  4G kwa  kweli  nafurahia sana" alisema  Bw, Mussa   Msemo  -Mtumiaji  wa  Mtandao  wa Tigo  4G

0 comments:

 
Blogs za Mikoa
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa