Na Pamela Mollel,Arusha
Imeelezwa
kuwa siku ya sheria ni siku ambayo wananchi wanapata fursa ya kupata
msaada wa kisheria ambayo kila mwananchi anapaswa kuwa chini ya shieria
na sio juu ya sheria.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake wakili wa kujitegemea Mruma
aShabibu kutoka kampuni IRM Legal alisema kuwa siku hii ni maalum kwa
mawakili kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila malipo yeyote.
Alisema kuwa
kwa siku hii watu wengi ufaidika kwa kutatuliwa baadhi ya matatizo yao
bila kutozwa gharama yeyote ikiwa ni pamoja na kupata elimu ya kisheria
sanjari na kupata fursa ya kubadilishana mawazo na mawakili.
Alidai kuwa
wananchi wanapaswa kuheshimu katiba lakini pia na kukaa chini ya sheria
ili haki iweze kutendekea kwani baadhi ya wananchi wanakaa juu ya sheria
hali ambayo inawafanya kujiona hawatendewi haki.
Hata hivyo alifafanua
kuwa lengo la kuanzishwa kwa siku hii ni kuangalia umuhimu wa sheria
katika jamii na kuona jinsi inavyofanya kazi katika kukuza uchumi wa
nchi
.Picha Wakili wa
kujitegemea Mruma aShabibu kutoka kampuni IRM Legal alisema kuwa siku
hii ni maalum kwa mawakili kutoa huduma za kisheria kwa jamii bila
malipo yeyote.
0 comments:
Post a Comment