Arusha
Home » , , » UVCCM LONGIDO YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA

UVCCM LONGIDO YATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA




Kushoto ni Katibu wa UVCCM wilaya ya Longido Isaya Karakara, Katibu Hamasa wa UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel na Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko w akikabidhi msaada kwa Mmiliki wa kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation Joyce Kabati .


Picha ya pamoja UVCCM wilaya ya Longido wakiwa katika kituo cha kulelea Watoto yatima cha Masai Foundation .Picha na Ferdinand Shayo




Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Longido umetembelea kituo cha Watoto yatima na Wanaoishi katika mazingira magumu cha Masai Foundation kilichopo mji mdogo wa Namanga na kutoa msaada wa vyakula pamoja na vifaa mbalimbali.

Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Robert Kaseko Amesema kuwa wameamua kushirikiana na jamii katika kusaidia watoto ikiwa ni moja kati ya michango wanayoitoa ili kutosheleza mahitaji muhimu yanayohitajika katika kituo hicho.

Robert Amesema kuwa jukumu la kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ni la kila mwanajamii hivyo jamii inapaswa kujitoa kusaidia watoto hao.

Katibu Hamasa wa CCM mkoa wa Arusha Neema Emmanuel amesema kuwa vijana hao wameamua kujitoa kutoa msaada kwa jamii ili kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hivyo ameiomba jamii kujitokeza kwa wingi kuwasaidia watoto hao.

“Hawa ni watoto wetu sote kila mtu anapaswa kuona kuwa ana jukumu la kuwasaidia hawa watoto ili waweze kufanikisha ndoto zao” Neema

Katibu wa UVCCM wilaya ya Londigo Isaya Karakara na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya Tulli Lemanga aliyejitolea kuwakatia bima ya afya watoto wanaolelewa katika kituo hicho wamesema kuwa vijana hao wataendelea na utamaduni huo mara kwa mara katika kuunga mkono juhudi za serikali katika kutatua changamoto za watoto.

Mmiliki wa kituo hicho Joyce Kabati amewashukuru vijana hao kwa kutembelea watoto hao jambo ambalo linaleta faraja kwa watoto hao ambao na wanamahitaji mbalimbali ambayo yamewasilishwa na vijana hao.


Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa