Na.Vero Ignatus Arusha.
Mahakama
kuu kanda ya Arusha imesikiliza maombi ya rufaa yayaliyowasilishwa na
upande wa jamhuri na ule wa mshtakiwa Godbless Lema ambapo pande zote
mbili wamekubaliana kusikilizwa rufaa ya upande wa jamhuri ambapo upande
wa serikali wameiomba mahakama kuwasilisha kwa hati ya maandishi hapo
kesho tarehe 30 disemba 2016
Aidha
rufaa hizo ni pamoja na ile ya upande wa Jamhuri kutoridhika na maamuzi
ya Jaji Dkt. Modesta Opiyo la kuwapa siku kumi (10) upande wa mshtakiwa
Lema kufaili notisi ya rufaa ,na upande wa mshtakiwa ni ile ya kupinga
uamuzi wa mahakama ya chini kushindwa kumpa Lema masharti ya dhamana
Jaji
aliyekuwa anasikiliza kesi ya rufaa hizo Salma Magimbi amesema kuwa
mara baada ya upande wa jamhuri kuleta rufaa kwa njia ya maandishi
upande wa mshtakiwa Lema wataijibu tarehe 30 desemba 2016 ambapo tarehe 2
januari watakutana pande zote kwa ajili ya kufanya majumuisho na
maamuzi ya rufaa hiyo yatatolewa tarehe 4 januari 2017
Hata
hivyo baada ya kusikiliza rufaa hizo mahakama imeibua hoja yenyewe na
kuwapa kazi mawakili wa pande zote mbili kuangalia kuwa notisi
iliyowasilishwa na mahakama ya chini imekidhi matakwa ya kisheria?
Kwa
upande wa wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala amesema kuwa kwa upande
wao wameiomba mahakama kusubirisha rufaa yao ili wasikilize kwanza rufaa
ya upande wa jamhuri kwani rufaa zote zimegongana na zinaelekea sehemu
moja
"Unajua
leo rufaa mbili zimegongana ile ya upande wa jamhuri na ile ya kwetu
sisi,hivyo basi sisis tumeiomba mahakama kusitisha rufaa yetui
isikilizwe ile ya serikali kwanza,kwani rufaa zote zinaelekea
upandemmoja ,wandege apande ndege na wa basi apande basi "alisema
Kibatala.
Hata hivyo mbunge huyo wa Arusha mjini Godbless Lema amerudishwa rumande hadi hapo maamuzi yatakapotolewa na mahakama.
0 comments:
Post a Comment