Nteghenjwa
Hosseah, Arusha
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dokta Frida Mokiti amesema kuwa uhaba wa vituo vya afya
katika maeneo ya pembezoni mwa miji umekua ukichangia vifo vya mama wajawazito
na watoto kutokana na kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.
Akizungumza
katika Kikao kazi cha Mkoa kinachojadili hali ya afya ya mkoa, Dr. Mokiti
amesema kuwa juhudi za makusudi zinahitajika kuhakikisha kuwa huduma za afya
kwa mama na mtoto zinapatikana kwa urahisi ili kupunguza tatizo hilo ambalo
limekua likirudisha nyuma afya ya wakina mama pamoja na kukatisha maisha yao.
Akizungumza
katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo amewaagiza Wakuu wa
Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha kuwa wanajenga Kituo cha Afya katika kila
tarafa ili kusogeza karibu huduma za afya kwa wananchi pia amewataka viongozi
kuweka mipaka katika maeneo ya zahanati ili kuepuka uvamizi wa maeneo hayo
yanayowahudumia watu.
“Wakati
sasa umefika wa kuhakikisha tunatokomeza kabisa changamoto hii ya vifo vya mama
na mtoto, inasikitisha sana kuona mama anafariki wakati wa kujifungua kwa
sababu tu amekosa huduma ya afya karibu na makazi yake,lazima tuwalinde na
kuwajali wananwake, kwa sababu bila ya wao kujifungua hata sisi tusingekuwepo”
Alisema Gambo.
Aliongeza
kuwa Kila Halmashauri ihakikishe inatenga Fedha kwenye mapato yake ya ndani
halkadhalika Ruzuku toka Serikali Kuu ielekezwe kwenye Miradi ya Afya na
tuendelee kutafuta wadau watakaotusaidia katika utekelezaji wa miradi hii bila
kusahau uhamasishaji wa nguvu za wananchi kwa Pamoja tutatokomeza tatizo hili.
Kwa
upande wake Mkazi wa Arusha Hussein Igunge na Mkuu wa Wilaya ya
Longido Mhe. Daniel Chongolo wameitaka serikali iboreshe huduma za afya
ikiwemo upatikanaji wa madawa kwa wale waliokata bima ili waweze kunufaika na
bima zao pamoja na uhaba wa watumishi katika sekta ya afya.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment