Mhe.Waziri
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyabiashara
wa Jiji la Arusha katika ukumbi wa AICC,Jijini Arusha.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo(kulia) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Lekule Laiza(kushoto).
Waziri
Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Mjaliwa amewata
wafanyabiashara kuwekeza zaidi kwenye sekta mbalimbali hasa za viwanda
hapa nchini.
Aliyasema
hayo alipokutana na wafanyabiashara wa jiji la Arusha nakuwashauri
wawekeze kwenye mikoa yote ya Tanzania hasa kwakuanzisha
viwanda,ilikujenga nchi ya viwanda kama dhamira ya serikali ilivyo.
“Nawashuri muwekeze kwenye mikoa yote hapa nchini na niruksa kabisa viwanda vingi vianzishwe”.
Hata hivyo amewata waendelee kushirikiana
na serikali yao ya awamu ya tano kwakuwa ipo pamoja nao na inaongeza
ulinzi zaidi kwa wafanyakazi wote nchini ili wawe na amani na waweze
kuwekeza zaidi.
Serikali
ya awamu ya tano itaendelea kuboresha zaidi kwenye sekta binafsi hasa
kwakupambana na wasiolipa kodi ili walipe nakuweka usawa katika biashara
na kukuza ushindaji wa biashara.
Aidha Majaliwa amewataka watendaji wa serikali kuvilinda viwanda vya ndani kwakuhamasisha matumizi ya
rasilimali za ndani napia kuzipunguzia ushuru ili viwanda viweze kukuwa
kwa kasi kama serikali inavyodhamiria kujenga nchi ya viwanda.
Majaliwa bado anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Arusha kwa kutembelea halmashauri zote za Mkoa.
0 comments:
Post a Comment