Arusha
Home » » UHAMIAJI WATAKIWA KUHAKIKISHA WANATHIBITI ONGEZEKO LA WATU KWA KUAJIRI UINGIAJI HOLELA WA WAGENI

UHAMIAJI WATAKIWA KUHAKIKISHA WANATHIBITI ONGEZEKO LA WATU KWA KUAJIRI UINGIAJI HOLELA WA WAGENI

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 


Na Woinde Shizza ,Arusha

Idara ya uhamiaji  imetakiwa kuhakikisha wanathibiti ongezeko la wakazi wa Tanzania ,kwa kuthibiti uingiaji holela wa wageni kutoka nje ya nchi.

Hayo yamebainishwa na Waziri mkuu Kassim Majaliwa wakati akiongea na watumishi wa Serikali wote wa halmashauri zote zilizopo ndani ya jiji la Arusha ambapo alisema kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la wageni ambao wanaingia nchini bila vibali huku wengine wakiwa awana shuhuli  ya msingi yakufanya.

Alisema  serikali imepanga bajeti ya wananchi kulingana na idadi ya wananchi wao ,sasa wanapo kuja wananchi kutoka nje bila sababu ya msingi na wanaoingia kiholela wanaingizia shida serial I pamoja na wananchi kwa ujumla

Alisema kuwa ni wajibu taasisi ya uhamiaji kuhakikisha wanakagua wageni wote wanaoingia na sababu gani na kuhakikisha anaeingia  kwani pia kumekiwepo na silaha nyingi zinazoingia  kiholela kutoka nchi za nje hivyo niwajibu wa tasisi hii kuhakikisha wanaoingia Wapo salama.

"Sasa ivi hawa wageni wakiingia waulizwe wanakuja kufanya nini kama ni kitalii walipie ada na uhamiaji wawapangie watakaa sikungapi ,kama anaingia kwa ajili ya biashara apangiwe Siku za kukaa na pia awa wanaokuja pia wachunguzwe wanakuja salama au anamambo yake mabaya"alisema Majaliwa

Aidha aliwataka maafisa uhamiaji wote kuhakikisha wanaimarisha ulinzi katika mipaka yote ,pamoja na kupita kwenye nyumba zote za wageni ili wajirithishe kama kweli wote waliolala umo ni watanzania na kama sio watanzania je wanavibali vya kuishi iwapo kama hawana hatua staiki zitatumika .


0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Arusha Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa