Benny Mwaipaja,
WFM, Arusha
Naibu Katibu Mkuu
Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Doroth Mwanyika, amewataka wakaguzi wa ndani
nchini kuhakikisha kuwa miradi mikubwa ya ujenzi wa miundombinu ikiwemo
barabara na majengo yanajengwa kwa ubora unaolingana na thamani ya rasilimali
fedha iliyotumika.
Bi. Mwanyika
ametoa rai hiyo Jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya wakaguzi
wa ndani kutoka Halmashauri za wilaya na Sekretarieti za mikoa iliyoko Kanda ya
Kaskazini, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara
Amesema kuwa
wabunge na wananchi kwa ujumla wamekuwa wakilalamikia miradi mingi mikubwa
ikijengwa chini ya kiwango na kuisababishia serikali hasara kubwa kutokana na
usimamizi mbovu unaofanywa na mamlaka na idara za serikali wakiwemo wakaguzi wa
ndani.
“Nina Imani kuwa
mafunzo mnayoyapata ya namna ya kukagua ubora wa miradi mikubwa inayotumia
fedha nyingi za serikali yatasaidia kuokoa fedha na kuifanya miradi inayojengwa
idumu muda mrefu” aliongeza Bi. Mwanyika.
Kwa upande wake
Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali Bw. Mohammed Mtonga, amesema kuwa kuanzishwa
kwa mafunzo hayo yanayofadhiliwa kupitia mradi wa kuboresha Mifumo ya Fedha
(PFMRP), yanatokana na mahitaji makubwa ya ujuzi wa namna ya wakaguzi wa ndani
wanavyoweza kutambua ubora wa miradi mikubwa ya ujenzi inayotekelezwa hapa
nchini kama inakidhi viwango.
“Wakaguzi hawa si
wataalamu wa masuala ya ukandarasi lakini uwezo wanaojengewa ni pamoja na
kupelekwa kwenye miradi mikubwa ya uejnzi ikiwemo barabaraba ambapo wataelekezwa
namna ya kutambua miradi ambayo haikidhi viwango na kutoa ushauri kwa watoa
maamuzi ili kuokoa fedha ya serikali isipotee” aliongeza Mtonga.
Wakaguzi wa ndani
302 kutoka Halmashauri na Sekretarieti za Mikoa nchini wamepatiwa mafunzo hayo
ambapo pamoja na mafunzo ya nadharia, wakaguzi hao wa ndani wamefundishwa
kivitendo namna ya kutambua miradi iliyojengwa chini ya viwango
Mwisho
0 comments:
Post a Comment