Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akizungumza na waendesha boda boda 200(hawapo pichani) watakaopatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba wakati wa kikao na vijana hao kukamilisha taratibu na masuala ya usalama kabla ya kukabidhiwa Pikipiki hizo.
Kijana muendesha boda boda(aliyesimama) akichangia kuhusiana na kiasi gani cha Fedha kirejeshwe kwa siku ili kukamilisha mkopo wa Pikipiki watakazopewa. Kwa wakati.
Umoja wa waendesha bodaboda Jiji la Arusha (UBOJA) wakiwa katika Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Arusha Bw. Charles Mkubwa
akitoa maelezo ya mafunzo ya udereva yatakayotolewa bure kwa vijana hao kuanzia tarehe 08/12/2016 kwenye Ukumbi wa
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Nteghenjwa Hosseah, Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amekutana wa waendesha boda boda 200
watakaonufaika na mradi wa kuwainua vijana kiuchumi katika Jiji la Arusha kwa
kupatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba.
Mhe. Gambo amekutana na vijana hao ili
kukamilisha taratibu za mwisho na kuangalia masuala ya usalama kabla
hawajakabidhiwa Pikipiki hizo.
Katika Kikao hicho vijana hao wamekubalina
kwa Pamoja kwamba watarejesha Tsh 7,000 kwa siku na pia na kwa atakayeweza kwa
wiki Tsh 49,000 ama kwa Mwezi itakua Tsh210,000.
Pia walikubaliana kwamba ni ruksa kwa yeyote
atakayeweza kulipia zaidi ya kiasi icho ili aweze kumaliza mkopo wa Pikipiki
yake na aweze kumilikshwa Pikipiki hiyo.
Haikatazwi kwa mtu yeyote kuleta zaidi ya Tsh
7,000 kwa siku ili uweze kumalizia mkopo wako mapema na ikitokea umekamilisha
mkopo huo hata kwa miezi miwili unamilikishwa Pikipiki alisema Mhe. Gambo.
Vijana hao pia walihoji kuhusu service ya
Pikipiki hizo na Mwakilishi wa Kishen Enterprises Ltd ambao pia ni mawakala wa
Pikipiki aina ya Toyo Mkoani hapa alisema Pikipiki hizo zina warrant wa meizi
sita na endapo zitapata hitilafu kwenye Engine katika kipindi hicho wataweza
kuifanyia matengenezo bila gharama yeyote au kubadilishiwa Pikipiki nyingine.
Kwa hesabu za kawaida vijana hawa watarejesha
Tsh 2,135,000 kwa mchanganuo ufuatao:
Tsh 2,000,000 ni Bei ya Pikipiki
Tsh 135,700 ni gharama ya Bima Kubwa hivyo
Vijana hao watarejesha Tsh 7,000 X siku 305 =
2,135,000.
Tunaposema watalipia kwa kipindi cha mwaka
mzima tunaamisha siku 60 zitakua kwa ajili ya service na dharura nyingine na
siku 305 ndio watakazoleta marejesho Alimalizia Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema Pikipiki hizo
zitakabidhiwa siku ya Jumamosi tarehe 10/12/2016 saa nne Asubuhi kwenye Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Wote Mnakaribishwa kushuhudia Tukio hili la
Kihistoria
0 comments:
Post a Comment