Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Shirika
la Umoja wa Mataifa la UN kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU)
wametoa Euro laki nane kuwasaidia watoto wa kike wanaoishi katika
mazingira magumu na wahanga wa mimba za utotoni waishio kwenye kituo cha
Faraja Young Women Development Unit .
Mwakilishi
wa EU ambaye ni Afisa Miradi Anna Muro amesema kuwa msaada huo
utasaidia kuwawezesha wanawake Waweze kushiriki kwenye maendeleo ya
jamii .
Akizungumza
katika kituo hicho kinacholelea watoto 30 wenye watoto ambao walipata
mimba katika umri mdogo na kushindwa kuendelea na masomo ambapo
wanasaidiwa na kituo hicho kupata elimu ya ufundi wa ushonaji na mapishi
ili kupata stadi zitakaowasaidia kujikwamua kimaisha.
Mwasisi
wa Shirika la Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara
akitoa maelezo kwa Maafisa wa UN na EU wakati walipotembelea kituo
shirika hilo. Kutoka kushoto ni Mwakilishi wa Mratibu Mkazi wa Mashirika
ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama, Mwakilishi wa EU ambaye ni
Afisa Miradi, Anna Muro (wa pili kulia) pamoja na Mtaalamu wa
Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu (kulia).(Picha
na Ferdinand Shayo).
Anna
amesema kuwa watoto wengi wanakabiliwa na changamoto ya usafirishaji wa
binadamu jambo ambalo ni kinyume cha haki za binadamu na haki za watoto
hivyo amewataka Jamii na serikali kupiga vita usafirishwaji wa watoto.
Mwakilishi
wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama
amewataka watoto wanaoishi katika kituo hicho kutumia fursa ya mafunzo
wanayoyapata kujiendeleza kielimu na kukua kiuchumi ili kutokomeza
umasikini na mimba za utotoni kwa watoto wa kike.
Muasisi
wa kituo hicho Martina Simon Siara ameshukuru ugeni kutoka UN na EU
uliofika kituoni hapo kwa ajili ya kutazama shughuli mbalimbali
zinazofanywa na kituo hicho pamoja na kuwaunga mkono ili waweze kuongeza
tija katika kuisaidia jamii.
Mwakilishi
wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama
(wa pili kulia) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro
(wa pili kushoto) wakipata maelezo kutoka kwa Muasisi wa Shirika la
Faraja Young Women Development, Martina Simon Siara (kulia)
walipotembelea shirika hilo lililopo jijini Arusha.
Wawakilishi
kutoka EU na UN wakitazama shughuli za mikono zinazofanywa na watoto
wanaoishi katika kituo cha Faraja Young Women Development Unit
walipotembelea kituo hicho hivi karibuni kilichopo jijini Arusha.
Mwakilishi
wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama
na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro wakishirikiana
kuingiza shanga ambazo hutumika kushona mavazi ya utamaduni yanayoshonwa
na watoto wa kike wanaoshi katika kituo cha Faraja Young Women
Development Unit (katikati) ni mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Rosemary
Innocent.
Binti mwenye ulemavu wa ngozi, Rosemary Innocent na wenzake wakiendelea na darasa la kutengeneza vitu mbalimbali kituoni hapo.
Mwakilishi
wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama
(kushoto) na Mwakilishi wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro katika
picha ya pamoja na binti aliyeshona vazi la kuvutia la kimasai
lililonakshiwa na shanga walipotembelea kituo hicho.
Wawakilishi wa UN na EU wakitazama kitengo cha elimu ya mapishi katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
wanafunzi wanaojifunza ushonaji katika Kituo cha Faraja Young Women Development Unit.
Mwakilishi
wa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Amon Manyama
akitazama mabinti wanaojifunza ushonaji nguo kituo cha Faraja Young
Women Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini
Arusha.
Mtaalamu
wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Hoyce Temu akifafanua
jambo kwa vijana na watoto wanaoishi katika kituo hicho walipokitembelea
jijini Arusha.
Mwakilishi
wa EU ambaye ni Afisa Miradi, Anna Muro akizungumza na wale, vijana
pamoja na watoto wanaoishi kwenye kituo cha Faraja Young Women
Development Unit walipokitembelea kituo hicho kilichopo jijini Arusha.
Wawakilishi wa UN na EU katika picha ya pamoja na walezi na watoto wanaoishi kwenye kituo hicho.
0 comments:
Post a Comment