Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Mtu
mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na
askari Polisi kisha kufariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya
Monduli kwa ajili ya matibabu.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo alipoongea na waandishi wa habari leo mchana
ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha,Naibu Kamishna
(DCP) Charles Mkumbo alisema tukio hilo lilitokea muda saa 07:00 Usiku
maeneo ya Makuyuni barabara ya Arusha-Makuyuni wilayani Monduli.
Kamanda
Mkumbo alisema jambazi huyo akiwa na wenzake wapatao 29 walikuwa na
bunduki ambayo bado haijafahamika pamoja na silaha za jadi mapanga na
marungu ambapo waliweka mawe barabarani na kulisimamisha gari aina ya
Fusso lenye namba za usajili T. 871 BUZ ambalo lilikuwa lina mzigo
likitokea Moshi kuelekea mkoani Singida.
‘’Mara
baada ya kulisimamisha gari hilo wakaanza kumpora abiria mmojawapo
aliyejulikana kwa jina la Victor Pius (46) Mfanyabiashara, mkazi wa
Majengo Moshi ambapo walichukua simu mbili aina ya Nokia na Samsung
pamoja na fedha taslimu Tsh 50,000/=’’.
“Wakati
wanaendelea na tukio hilo askari Polisi waliokuwa High Way Patrol
walipata taarifa za tukio hilo ambapo walikwenda kwa haraka na mara
baada ya majambazi hao kuwaona walianza kufyatua risasi hovyo na Polisi
kuanza kujibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi mmojawao na kuwakamata
wengine kumi na mbili papo hapo wakiwa na mapanga sita na marungu manne
huku wengine akiwemo na yule mwenye bunduki wakikimbia”. Alifafanua
Kamanda Mkumbo.
Kamanda
Mkumbo alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huu kuendelea kushirikiana na
Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu ili zifanyiwe kazi kwa
haraka, huku akitoa onyo kwa majambazi wanaopenda kujipatia kipato bila
kuvuja jasho kwani Jeshi hilo limejiandaa vizuri.
0 comments:
Post a Comment