Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Mashaka Gambo akihutubia wananchi wa kijiji cha Esilalei katika tarafa ya Makuyuni Wilayani Monduli.
Mkurugenzi Mtendaji wa Africa Wildlife Foundation akisoma taarifa fupi ya mradi wa shamba la Manyara Ranch kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo(hayupo pichani),pembeni yake kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Richard Kwitega akifuatilia taarifa hiyo.
Wananchi wa kijiji cha Esilalei wakiwa kwenye mkutano wa hadhara ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akijibu hoja mbalimbali za wananchi wa Makuyuni alipofanya ziara katika tarafa hiyo iliyopo Wilayani Monduli.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo ameiagiza halmashauri ya Wilaya ya
Monduli Mkoani Arusha kupitia upya taratibu na kanuni zilitumika kwenye
umiliki wa shamba la Manyara Ranch lililopo tarafa ya Makuyuni.
Alisema
hayo alipofanya ziara ya siku moja katika tarafa hiyo nakutembelea
shamba la Manyara Ranch ambalo wananchi wanadi ni mali yao baada ya
umiliki wake kufutwa mwaka 1999 nakurudishwa kwa wananchi.
Hata hivyo bado kuligubikwa na maswali mengi ya hati miliki ya shamba kuandikwa jina la Tanzania Land Conversation Trust (TLCT) ambacho
ni chombo cha kusimamia shamba hilo na badala ya mmiliki mkuu ambae ni
Halmshauri ya Wilaya ya Monduli, hali iliyopelekea Gambo kutolea maamuzi
ya hati miliki iandikwe Halmashauri ya Wilaya ya Monduli.
“Naiagiza
Halmashauri kuhakikisha hati miliki ya shamba hili isomeke jina la
Halmashauri badala ya TLCT kwasababu tayari shamba lilisharudishwa kwa
wananchi na halmashauri ndio msimamizi wa mali za wananchi”,alisema.
Akisoma
taarifa fupi ya shamba la Manyara Ranch Mkurugenzi mtendaji wa taasisi
ya African Wildlife Foundatio(AWF)ambao ndio wanaendesha shughuli zote
katika shamba hilo bwana Fidelisi Ole Kashe amesema taasisi hiyo
iliingia mkataba wakuendesha shughuli zote ndani ya shamba kutoka kwa
TLCT baada ya chombo hicho kushindwa kuziendesha.
Aidha
akifafanua zaidi Mkurugenzi mtendaji wa TLCT bwana Boniface Ngimojiro
alisema TLCT iliundwa na bodi ya halmashauri ya wilaya ya Monduli ili
isimamie na kuendesha shughuli zote za shamba la Manyara Ranch na baada
yakushindwa kuendesha ndipo wakazikabidhi kwa AWF.
Hata
hivyo Gambo alisema ataunda timu yakuchunguza shughuli zote za TLCT kwa
mda wa miaka 10 ya nyuma ilikusaidia kufahamu zaidi kama chombo hicho
bado kinahitajika katika uwendeshaji na usimamizi wa shughuli za shamba
la Manyara Ranch.
Gambo
amekuwa akifanya ziara zake katika wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha
kwa lengo lakusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazowakabili.
0 comments:
Post a Comment