Picha ikionyesha wa kwanza kushoto mwimbaji wa
zamani wa bendi ya FM
academia Kingombe Mohamed (kingblez) akisaini mkataba wa miaka mitano
wa kufanyakazi katika bendi mpya ya East African Gwasuma music band
ilipo jijini Arusha anayefata wa kwanza kulia ni wakili wa
bendi hiyo
Vivianus Rugakingira wanyuma wa kwanza ni mkurugenzi wa bendi hiyo
Muktar Abdu Bolydo (Obama) na wafanyakazi wake wakishuhudia king blez
akisaini mkataba wa kufanyakazi katika bendi hiyo kwa miaka
mitano
Afisa utamaduni wa jiji la Arusha Benson Maneno akimkabidhi KIng blez mkatabawake mara baada ya kusaini
Meneja wa bandi akifatilia kwa makini mkataba
wa wasanii hao
baadhi ya wasanii wa bendi ya East African gwasuma music band
Na Woinde
Shizza,Arusha
WASANII
mbalimbali jijini hapa wanatarajiwa kuanza kupata neema ya kukuza
vipaji vyao baada ya bendi mpya ya muziki kuanzishwa.
Bendi hiyo mpya
'East African ngwasuma music band itakuwa ikifanya kazi zake jijini
hapa.
Mkurugenzi
wa bendi hiyo ya East African Ngwasuma Music bendi Mukhtar Abdul Bolydo
(Obama) alisema ni fursa kwa vijana wenye vipaji vya sanaa ya muziki
katika uimbaji kujitokeza ili kuwania nafasi katika bendi
hiyo.
"Hivi
sasa tumeanzisha bendi hii bado tunauhitaji wa vijana wasiopungua 20
kwani malengo yetu ni kuwa na bendi mbili hapo baadaye na ni wakati wa
Arusha kupata burudani ya aina yake",alisema Abdul.
Alisema
bendi hiyo itaongozwa na msanii nguli wa muziki kutoka Fm Academia
ambaye amehama na kujiunga na bendi hiyo mpya kwa kiasi cha shilingi
Milioni 20 na amesaini mkataba wa miaka mitano wa utoaji wa huduma ya
muziki.
Msanii
huyo 'King of the king'king'(mzee wa mujini) Kingombe Mohammed alisema
ataitumikia bandi hiyo kwa ajili ya kutoa burudani.
"Nimekuwa
FM Academia kwa miaka mingi hivi sasa nimehama na tumeamua kuanzisha
bendi mpya itakayokuwa moto wa burudani,".alisema
Mohammed.
Bendi
hiyo mpya ya East African Ngwasuma Music bendi yenye makao yake makuu
jijini hapa, ina jumla ya wasanii 12 kati yao wawili wanawake na kila
msanii ana mkataba wa miaka miwili na baada ya hapo kama atafanya vizuri
ataendelea kutumikia kulingana na uwezo wake.
0 comments:
Post a Comment