Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akikabidhiwa Zawadi na Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC) Joseph Mayagila katika Mahafali ya chuo hicho yaliyofanyika chuoni hapo
Wahitimu wa Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) wakirusha kofia juu ishara ya kuonyesha kutunukiwa vyeti vya Shahada na Stashahada.
picha ya pamoja na wahitimu
Meya wa Jiji la Arusha Kalisti Lazaro akimtunuku cheti cha stashahada ya Uandishi wa Habari na Utangazaji Editha Makundi wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC),wawatu kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo wa Chuo cha Arusha Journalism Training College (AJTC) Joseph Mayagila.
Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro akizungumza katika Mahafali ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Arusha (AJTC) ,Kulia ni Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo hicho Joseph Mayagila,kushoto ni Diwani wa kata ya Themi ,Melans Kinabo.Picha na Ferdinand Shayo
Meya wa Jiji
la Arusha Kalisti Lazaro amewatunuku zaidi ya wahitimu 50 waliohitimu katika
Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji
(AJTC) huku akiwataka kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za
jamii na kuleta mabadiliko kupitia kalamu zao.
Kalisti
amewataka Wanahabari kujikita katika kuandika habari za kijamii zitakazosaidia
kutatua changamoto zinazoikabili jamii na kuleta suluhu kwenye matatizo ya
jamii.
Ameishauri serikali
kuangalia upya mswada wa habari na kuufanyia marekebisho katika vipengele
ambavyo vinaminya haki ya habari.
Mkurugenzi
wa Mafunzo katika Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji ,Joseph Mayagila
amesema kuwa tasnia ya habari ni tasnia muhimu katika kuchochea maendeleo ya
nchi kwani bila taarifa hakuna maendeleo.
Alisema kuwa
ni vyema serikali ikatazama upya utekelezaji wa sheria mpya na kufanyia kazi
mapungufu ili wanahabari waendelee kuwahabarisha Watanzania.
0 comments:
Post a Comment