Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo
akiongea na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo,amewataka watumishi wote wa Mkoa wa Arusha kutekeleza
wajibu wao kama watumishi na kuachana na mambo ya siasa ambayo yanarudisha maendeleo yawananchi nyuma. |
Ameyasema hayo alipokuwa akiongea na
watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro alipofanya ziara ya siku moja
Wilayani humo na kukutana na changamoto mbalimbali zikiwepo za migogoro ya
ardhi.
Muheshiwa Gambo ameziagiza
Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kuhakikisha inatatua migogoro yote ya ardhi
na ile inayoshindikana kwa ngazi hiyo ndio ipelekwe kwenye ngazi ya Mkoa na
yeye atakuwa tayari kuwasaidia.
Aidha ametaka kupewa ripoti ya fedha
zinazotolewa na wafadhili katika kila Halmashauri napia zile zinazopelekwa kwa
wafugaji zielezwe matumizi yake na yeye atapita kukagua hizo shughuli za
maendeleo kwa wananchi ili ajiridhishe na matumizi yake kama ni halali au sio.
Alisema anataka kupata pia taarifa
juu ya chakula kinachotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa wananchi
wa Wilaya hiyo kama kweli kinawafikia wahusika hususani wananchi wa hali ya
chini.
"Ikibainika kuwa fedha za
wafadhili na chakula cha msaada vyote vinatumika visivyo basi wahusika
wajiandae kuwajibishwa ipasavyo, kwasababu tunatakiwa kuwatendea haki wananchi
wetu na sivinginevyo",alisema Gambo.
Aidha aliwaomba wawekezaji
wakishirikiana na madiwani waendelee kudumisha uhusiano mzuri baina ya wananchi
na wawekezaji hao ili kwa pamoja maendeleo kwa wananchi yapatikane kwa wakati.
Muheshiwa Gambo alikuwa na ziara ya siku moja katika Wilaya ya Ngorongoro kwalengo lakufuatilia shughuli mbalimbali za maendeleo kwa wananchi.
0 comments:
Post a Comment