Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho
Gambo,awataka viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro kuchagua eneo maalumu kwaajili
ya ujenzi wa ofisi za forodha katika mpaka wa Ngorongoro na nchi ya Kenya.
Ameyasema
hayo alipo tembelea eneo la mpaka wa nchi ya Kenya na Tanzania kwa upande wa
Wilaya ya Ngorongoro akiambatana na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya mapato
Tanzania(TRA) Bwana. Alphayo Kidata. "Nawaagiza Viongozi wote wa
Wilaya hii kuanzia Mkuu wa Wilaya,Mwenyekiti wa Halmashauri na diwani wa
Kijiji cha Njoroi kukaa na wananchi nakisha kuamua ni eneo gani ambalo litafa
kujenga ofisi zetu za forodha".
|
|
Alisema Serikali ya awamu ya tano
ipo karibu sana na wananchi wa hali ya chini hususani katika kuwaletea maendelea
hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana kikamilifu na Serikali yao. Amesema
Serikali imeona kuna ulazima wakujenga ofisi za forodha katika Kijiji hicho ili
kujipatia mapato kutoka kwa wageni wanaoingia na pia kupunguza uwingizaji wa
mifugo kiholela.
Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa na
Kamishina Mkuu wa TRA katika Wilaya ya Ngorongoro hususani katika Kijiji cha
Njoroi ilikuwa na lengo lakuona ni eneo gani litafaa kuwa na ofisi za
forodha ambapo litapunguza uwingiaji wa wageni kutoka nchi jirani ya Kenya ambao
wanaingia nchini Tanzania kwalengo lakujipatia mahitaji mbalimbali bila
yakutozwa kodi.
0 comments:
Post a Comment