Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, akimsikiliza mratibu wa mradi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi Bwana Alize Morengati,alipokuwa akiuwelezea mradi huo kwa viongozi mbalimbali wa Mkoa katika ofisi ya Mkoa.
Mradi
wa kukuza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi
unatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwaka huu. Kwa Mkoa wa Arusha, mradi huu
utawanufaisha wafugaji wa Wilaya tatu za Monduli, Longido na
Ngorongoro.
Lengo
la Mradi wa kukuza uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya
tabia nchi ni kuziwezesha Wilaya kukabiliana na mabadiliko ya tabia
nchi, hususani jamii za kifugaji.
Mradi
utawezesha maeneo kame (dry lands) kupata njia mbadala ya ustahimilivu
kutokana na mabadiliko ya tabia nchi katika kuchangia usalama wa chakula
na uchumi imara wa wananchi.
Vilevile kuwezesha wana jamii ya kifugaji kupanga mipango yenye kuzingatia matumizi bora ya Rasilimali walizonazo.
Mambo
muhimu yanayozingatiwa katika mipango hiyo ni pamoja na upatikanaji wa
maeneo ya malisho na upatikanaji wa maji unaozingatia utawala wa maeneo
na usuluhishi wa migogoro juu ya matumizi ya Rasilimali.
Mradi
huu utawezesha halmashauri hizi tatu kuandaa mipango ya miradi ya
maendeleo itakayoweza kukabiliana na athari za tabia nchi katika jamii
hizi za wafugaji.
Shirika
la Hakikazi Catalyst na Taasisi ya Kimataifa ya Mazingira na Maendeleo
(IIED) yatashirikiana na halmashauri hizi tatu kuwezesha mradi huu kwa
halmashauri tatu za Mkoa wa Arusha kwa muda wa miaka mitano kuanzia 2016
hadi 2021.
0 comments:
Post a Comment