Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo,aiagiza Mamlaka ya uthibiti wa usafari
wa majini na nchi kavu (SUMATRA) kuendelea kutoa leseni za magari aina ya Noha kwa Mkoa wa Arusha,hasa kwa yale yanayofanya safari zake kati ya Arusha mjini kuelekea Karatu na Longido.
Aigizo hilo
amelitoa baada yakupata malalamiko kutoka kwa uwongozi wa wamiliki wa
magari hayo ukiongozwa na wenyekiti wake Bwana Ally Mkali alisema
SUMATRA wamesitisha utoaji wa leseni za kawaida kwa magari ya Noha na wataanza kutoa leseni kwa yale yatakayokuwa tayari kutembea umbali wa Kilometa 50 tu.
“Nawaagiza
SUMATRA kuendelea kutoa leseni kwa utaratibu uliopo kwasasa na wakati
huo mjipange kukutana na wadau wote nakujadili namna yakulitatua swala
la magari haya kutembea umbali wa Kilometa 50 hasa kwakuangalia mazingira ya Mkoa wa Arusha nimagumu na kwakulitekeleza hilo litaongeza gharama kwa wananchi”,alisema Gambo.
Mkurugenzi
wa mamlaka hiyo kwa Mkoa wa Arusha Bwana Allen Mwanri, alisema sababu
zilizopeleka SUMATRA kupitisha utaratibu huo kwa magari hayo ni kutoweza kumudu kutembea umbali mrefu kwani ni hasara napia inahatarisha maisha ya abiria.
“Tuliamua kupendekeza utaratibu huu kwasababu magari mengi ya Noha yalionyesha kushindwa kutembea umbali mrefu na huku yakibeba abiria zaidi yakiwango kinachoitajika cha watu nane”,alisema Mwanri.
Aidha
Mkuu wa kikosi cha usalama barabara Mkoa kamanda Nuru
Selemani,amewataka madereva wa magari hayo aina ya Noha kufuata sheria
na taratibu za barabarani ilikulinda usalama wao na abiria,na
kwakushindwa kufanya hivyo basi sheria zitachukuliwa dhidi yao.
Maamuzi hayo yalitolewa baada ya Mkuu wa Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa kuwatembelea madereva wa magari hayo maeneo ya standi kuu
ya Mkoa nakujionea hali halisi ya utoaji huduma kwa magari hayo kwani
mengi yalikuwa yamesitisha huduma hiyo kwakukosa leseni za usafirishaji.
0 comments:
Post a Comment