RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefanya
mabadiliko madogo ya uongozi na kumteua Bw. Mrisho Gambo kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Arusha kuanzia leo (Alhamisi, Agosti 18,2016).
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Bw. Gambo anachukua nafasi ya aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Felix Kijiko Ntibenda ambaye uteuzi wake
umetenguliwa.
Amesema Bw. Ntibenda anahamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambako atapangiwa majukumu mengine.
Kabla
ya uteuzi huo, Bw. Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha. Ataapishwa
kesho (Ijumaa, Agosti 19, 2016) saa 3 asubuhi Ikulu jijini Dar es
Salaam.
0 comments:
Post a Comment