Naibu Waziri wa Habari Utamaduni , Sanaa na
Michezo akikabidhi vyeti vya usajili wa
Chama cha Madijey nchini leo jijini Arusha kwa Mwenyekiti wa Chama hicho
Bw.Yusuph Juma kuashiria uzinduzi wa chama hicho rasmi.
Na Anitha Jonas –
MAELEZO
Arusha.
Wasanii wa wanofanya
kazi ya u-dijey watakiwa kujisajili
katika Chama kwa lengo kujenga misingi imara ya taalum hiyo.
Hayo yamesemwa leo
Jijini Arusha na Naibu Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo alipozindua
chama hicho rasmi katika mkutano wa wadau wa kisekta uliyofanyika katika ofisi za Mkuu wa Mkoa ambapo alikutana
na wadau mbalimbali.
“Kuanzishwa kwa chama
hiki kuanashiria ni kwa kiasi gani wadau wa sekta ya sanaa wameelewa umuhimu wa
kurasimisha kazi zao na hili litaongeza tija katika kujenga heshima ya kada hii
ya madijey katika nchi yetu kama
ilivyokwa nchi zilizoendelea”,alisema Naibu Waziri Wambura.
Kwa upande wa
Mwenyekiti wa Chama cha Madijey Bw.Yusuph Juma alisema wameamuo kuanzisha chama
hicho cha madijey kwa kuwa sanaa hiyo imekuwa ikidharaulika kwa kiasi kikubwa
imekuwa ikionekana kama siyo sekta rasmi bali ni uhuni .
“Usajili wa madijey
katika chama utazingatia vigezo vya taalum pamoja na leseni za udijey hii ni kwa lengo la kuimarisha sekta hii ili kuipa
nguvu na kuifanya iheshimike kama kazi nyingine za kisana na
sivinginevyo”,alisema Bw.Juma.
Pamoja na hayo
Mwenyekiti huyo alisema madijey wengi nchini wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa
kulipwa ujira mdogo ukilinganisha na masaa wanayokuwa wakifanya kazi hiyo,hivyo kwa kupitia umoja huo wataunda
muongozo utakaosaidia kuboresha mazingira ya malipo yao.
Pia Bw.Juma
ameiomba serikali kusimamia suala la
madijey wote nchini kujiunga katika chama hicho kwa lengo la kuunda umoja wao
utakowasaidia kupata fursa mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo kutafuta namna
ya kuongeza maslai
yao.
Hata hivyo uongozi
huo umetoa shukrani kwa Serikali kwa ushirikiano uliyowapa katika kupitisha
chama hicho ambacho kimesajili katika Baraza la Sanaa la Taifa .
0 comments:
Post a Comment