Anitha Jonas –
MAELEZO
Arusha.
Serikali ya pongeza
uongozi wa Trust St.Patrick Sport Academy
kwa uamuzi wa kujenga Kituo cha
Mafunzo ya Michezo chenye hadhi ya
Kimataifa.
Pongezi hizo
zimetolewa leo jijini Arusha na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na
Michezo Mhe. Anastazia Wambura alipotembelea eneo hilo litakalojengwa kituo
hicho ambacho kitakuwa na Michezo ya aina mbalimbali pamoja na hoteli ya nyota
tano.
“Serikali inaunga
mkono jitihadi za ujenzi huu kwani kituo hichi kitakapo malizika tunaimani
kitakuwa chachu ya ukuaji wa vipaji vya
michezo kwa watanzania na kutaongeza mafanikio ya sekta ya michezo na kuwezesha
kupata ushindi katika michezo mbalimbali katika ngazi za Kimataifa,”alisema
Naibu Waziri.
Naye Katibu Mkuu wa
Kituo hicho Bi.Dinna Patrick alimweleza
Naibu waziri huyo chagamoto waliyonayo
katika eneo hilo la kuwepo kwa barabara inayogawa eneo hilo la kituo
hicho ambalo ndiyo limekuwa kikwazo kinacho kwamisha ujenzi wa kituo hicho
kuanza kwa haraka.
“Kituo hicho kitakuwa
na uwanja wa mpira ambao utakuwa na uwezo wa kuchukua watu elfu ishirini ambao
utakuwa wenye hadhi ya kimataifa na kituo hicho kinatarajiwa kuwa bora zaidi
katika Kanda ya Afrika
Mashariki”,alisema Bi.Patrick.
Baada ya kupata
malalamiko hayo Mheshimiwa huyo aliuagiza uongozi wa mkoa kufuatilia suala hilo katika ofisi za
Halimashauri na kusaidia suala hilo kupata ufumbuzi ili kuharakisha ujenzi wa
eneo hilo kwani kumalizika kwake kutaleta faida kubwa kwa wapenzi wa michezo.
Aidha ,Naibu waziri
huyo alitoa wito kwa uongozi wa Trust St.Patrick Sports Academy kujenga pia
chuo cha walimu wa michezo mbalimbali nchini kwani kuna changamoto kubwa ya
ukosefu wa walimu wa michezo na uhaba wa vyuo vya michezo nchini.
Hata hivyo watanzania
wenye uwezo wametakiwa kujitokeza na kujenga vituo vya mafunzo ya michezo kwani
michezo ni ajira na inaweza kuchangia pato kubwa katika nchi.
0 comments:
Post a Comment