Na Raymond Mushumbusi MAELEZO.
Wabunge wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wamelaani mauaji ya mbunge mwenzao kutoka Burundi Bi. Hafsa Mossi yalitokea leo kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni Jijini Bujumbura.
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kutokea kwa tukio hilo mbunge wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki na Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Kikanda
na Usuluhishi wa Migogoro kutoka katika Bunge hilo Mhe. Abdallah Mwinyi
amesema kuwa, kitendo cha kuuawa kwa mbunge huyo si cha haki hata
kidogo kwa kuwa mbunge huyo hakuwahi kujihusisha na migogoro wa aina
yoyote katika nchi hiyo.
“Tunalaani
kwa nguvu zote mauaji ya mbunge mwezetu kwani ni kitendo cha kinyama na
tunatoa wito kwa Waasi kusitisha ghasia na kukaa katika meza ya
mazungumzo kutafuta suluhu” Alisema Mhe. Mwinyi.
Kwa
upande wake Mhe. Nderakindo Kessy Mbunge wa Afrika Mashariki na
Mwenyekiti Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo ameongeza kuwa wamesikitishwa
na mauaji hayo ya kikatili aliyofanyiwa Mbunge mwenzao na kuomba haki
itendeke na kuwapata wale ambao wamehusika na mauaji hayo na kuchukuliwa
hatua za kisheria.
“Tunasikitika
sana na mauaji yalitokea kwa mbunge mwenzetu lakini naahidi kuendeleza
yale aliyoyaacha Mhe.Hafsa Kessy hasa katika kupambana katika haki za
wanawake na watoto” Alisisitiza Mhe. Nderakindo.
Mhe.
Hafsa Mossi aliwahi kuwa Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika
Serikali ya Rais Pierre Nkurunziza na mtangazaji maarufu wa idhaa ya
Kiswahili ya shirika la utangazaji la BBC.
0 comments:
Post a Comment