Zhakaria ni shahidi wa 10 wa kesi ya uchaguzi Jimbo la Longido mkoani
Arusha, alitoa ushahidi wake mahakamani mjini hapa mbele ya Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Bukoba, Silvangirwa Mwangesi.
Mtaalamu huyo wa kompyuta ambaye inadaiwa ndiye aliyekuwa akiingiza
kura za fomu 21b za vituo vyote 175 katika jimbo hilo kwenye kompyuta
kuu ya tume, alisema hayo wakati akihojiwa na Wakili Edmung Ngemela
mbele ya Jaji Mwangesi.
Alidai mfumo mkuu wa Tume ya Uchaguzi wa uingiza kura kutoka katika
vituo 175 vya jimbo la Longido uliposhindwa kufanya kazi kila kitu
kilikuwa ni matatizo. Shahidi huyo alidai waliamua kurudia kuhesabu
zaidi ya mara tatu lakini matatizo hayakumalizika.
Alidai hata hesabu ya mwisho iliyomtangaza mgombea wa Chadema, Onesmo
ole Nangole kuwa mshindi ulikuwa na matatizo na kasoro za kimahesabu.
Pia shahidi huyo alikiri mahakamani hapo kuwa hata hesabu zilizokuwa
katika kiapo chake zinatofautiana na zilizotangazwa na kumpa ushindi
Nangole kwani kasoro za kimahesabu zilikuwa nyingi na zilitofautiana.
Shahidi wa 11 Sinyak Merita (48) ambaye alikuwa msimamizi msaidizi wa
uchaguzi kata ya Kamwanga wilayani Longido mkoani Arusha yeye alidai
hakukuwa na malalamiko ya raia kutoka nchi jirani ya Kenya kwamba
walikwenda kupiga kura katika kata yake kuanzia kujiandikisha hadi
uchaguzi.
Alidai hakukuwa na malalamiko yoyote juu ya kuwepo kwa Wakenya katika
kata hiyo na kama kuna shahidi alisema walikuwepo yeye hakuwa anawajua.
Merita alikiri kutowakagua watu waliokuwa wamejiandikisha katika
daftari la kupiga kura kwani aliamini kuwa waliojiandikisha wote
walikuwa raia wa Tanzania na wenye miaka zaidi ya 18.
Shahidi wa 12 ,Tito Mndeme {51} msimamizi kata ya Kimokowa yeye
alisema kuwa alisimamia vituo 11 vya kata hiyo na alihusika kubandika
majina ya watu waliojiandikisha katika vituo vyote.
Mndeme ambaye ni mwalimu wa shule ya msingi kwa miaka 27 alisema kuwa
alihusika kusimamia uandikishaji lakini hakusikia malalamiko kama
kulikuwa na watu raia kutoka nchi jirani ya Kenya walijiandikisha na
kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka jana.
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Longido ambaye ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Longido, Felix Kimario anatarajiwa kutoa ushahidi wake
leo na kufunga ushahidi wa upande wa mjibu maombi. Mwanasheria wa
Serikali, David Akway alimweza Jaji Mwangesi kuwa Mkurugenzi atakuwa
shahidi wao wa mwisho hivyo watakuwa wamefunga ushahidi wao .
Chanzo Gazei la Habari Leo
0 comments:
Post a Comment