Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

Waziri
wa TAMISEMI George Simbachawene akizungumza jana katika Mkutano wa nane
wa wadau wa LAPF unaoendelea jijini Arusha katika ukumbi wa AICC ambapo
alikuwa mgeni rasmi mbali na mambo mengine,aliitaka mifuko ya hifadhi
ya jamii kutoa mafao kwa wakati pindi wanachama wake wanapostaafu ili
kuhakikisha kuwa wastaafu wanapata mafao yao, kwani wengi wao
wanakabiliwa na msongo wa mawazo kutokana na ugumu wa maisha
unaowakabili baada ya kustaafu wanashindwa kujimudu kutokana na kukosa mafao yao(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)

Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama
ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kuunga
mkono msimamo wa serikali kuanzisha uchumi wa viwanda utakaotengeneza
ajira na kuchochea maendeleo ya nchi

Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa Mifuko
ya hifadhi ya jamii imekua chachu ya maendeleo ya taifa kutokana na
uwekezaji unaofanywa na mifuko hiyo pamoja na mikopo mbalimbali
inayotolewa kwa wanachama kujikwamua kimaisha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha

Afisa
Masoko wa LPF James Mlowe akizungumza katika mkutano huo ambapo
alisema kuwa tayari mfuko huo umeanzisha mkopo wa maisha popote na LAPF
ambao unalenga kuwasaidia watumishi wa umma hususan wale walioajiriwa
maeneo ya vijijini ili waweze kuanza maisha na kuwatumikia watanzania
bila vikwazo vya kiuchumi…

Makamu mwenyekiti wa bodi Husein Kamote
alisema mfuko huo unakabiliwa na changamoto nyingi zinazokwamisha
utekelezaji wa mipango yake ikiwemo deni inalolidai serikali ambalo
halijalipwa kwa mda mrefu huku likizidi kuongezeka

Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akiteta jambo na Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga

Wadau katika mkutano
Mdau kutoka benki ya NMB akizungumza katika mkutano huo

Mwandishi wa habari wa star tv Ramadhan Mvungi akifatilia mkutano kwa ukaribu

Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akipokea zawadi ya saa aliyokabidhiwa na mfuko huo

Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama akipokea zawadi ya saa aliyokabidhiwa na mfuko huo

Waziri wa TAMISEMI George
Simbachaweneakimkabidhi kaimu mkurugenzi Geita John Muta hundi ya
shilingi milioni saba tu baada ya halmashauri hiyo kufanya vizuri na
mfuko huo

Wadau wakifatilia mkutano

Wadau kutoka mifuko mingine pia walishiriki mkutano huo

Mnufaika wa LAPF kupitia maisha popote
Scolastika Francis kutoka Kilolo ambaye ni mwalimu akitoa ushuhuda jinsi
mkopo huo ulivyoweza kubadili maisha yake ambapo sasa anamiliki nyumba
pamoja na shamba mbali na ajira yake

Mwalimu wa shule
ya sekondari Rombo Njuguna Rombo akitoa ushuhuda jin si mfuko huo
ulivyoweza kubadili maisha yake ambapo ameweza kununua kiwanja huku
akimiliki mradi wake wa kuku
0 comments:
Post a Comment