Mahmoud Ahmad Arusha
SERIKALI
imefuta hati za mashamba makubwa 13,ambayo kwa muda mrefu yamekuwa
hayaendelezwi na kuyakabidhi kwa uongozi wa wilaya ya Monduli ili
yagawiwe kwa wananchi ambao hawana ardhi.
Shughuli
hiyo ya kukabidhi mashamba hayo imefanyika kwenye kata mbili za
Lokisale na Olmot ,wilayani Monduli, kwenye mkutano wa hadhara .
Waziri
wa Ardhi na Maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi, amesema mashamba hayo
yalikuwa yakimilikiwa na wawekezaji ambao hawayajaendeleza kwa kipindi
kirefu yapo vijiji vya Mswakini na Lokisale.
Aidha
waziri Lukuvi ameuagiza uongozi wa halmashauri ya Monduli, kumpatia
orodha ya mashamba mengine 39,ambayo hayajaendelezwa kabla ya mwosho wa
Marchi mwaka huu ili nayo yafutiwe hati na kuyagawa kwa wananchi ambao
hawana mashamba wilayani humo.
Waziri
Lukuvi, amesema kuwa serikali inawahitaji wawekezaji wa kweli ambao
watayaendeleza maeneo lakini sio ambao wameyatelekeza mashamba hguku
wananchi wakikosa mashamba ya kulima .
Waziri,
Lukuvi,amesema uwekezaji kwenye mashamba lazima uambatane na utoaji wa
ajira za kudumu na sio vibarua na ajira iwe ni chanzo muhimu na
kusisitiza wawekezaji ambao hawataki kutoa ajira warudishe ardhi hiyo
waliyoimiliki.
Amewaambia
kuwa ardhi ambayo mwekezaji ameshindwa kuiendeleza ikifutiwa umiliki
wake haitalipwa fidia kwa kuwa mhusika ameshindwa kuiendeleza na
ameitelekeza.
Waziri,
amesisitiza kuwa kipaumbele cha ardhi inayofutiwa hati miliki ni kwa
wananchi maskini na sio wenye uwezo, wenye ardhi au viongozi la hasha
bali kipaumbele ni kwa wale ambao hawana kabisa ardhi.
Aidha
amezuia maafisa ardhi ngazi za kanda nchini kutokujihusisha na
uhamishaji wa umiliki wa ardhi na mashamba au kusajili mashamba mapya na
kutoa hati miliki mpaka waziri ataarifiwe kwanza.
Amesema
amegundua kuna ujanja ujanja, unaotumiwa na wamiliki wa mashamba ambao
huyauza na kusajili maeneo yaliyobakia jambo ambalo ni kinyume na
sheria.
0 comments:
Post a Comment