Na Lilian Lundo – Maelezo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha SACP
Liberatus Sabas amekanusha habari iliyoandikwa na gazeti la Jambo Leo
la Januari 27, 2016 lenye kichwa cha habari “Waendesha bodaboda Arusha
waandamana.
Akiongea
kwa njia ya simu Kamanda Sabas alisema hakukuwa na maandamano yoyote ya
bodaboda jijini Arusha zaidi ya vijana wachache waendesha bodaboda
waliojikusanya kwa Mkuu wa Mkoa.
Kamanda Sabas amesema kuwa, wapo katika operesheni ya waendesha bodaboda ambao wamekuwa wakivunja sheria za barabarani mara kwa mara. Operesheni hiyo ni ya nchi nzima na wameianza Januari 14, 2016.
“Mpaka
sasa tumekusanya sh. mil. 21,330,000 ambazo zimetokana na makosa
mbalimbali yanayofanywa na waendesha bodaboda wawapo barabarani, makosa
hayo ni kutovaa kofia ngumu, kutokuwa na leseni ya udereva, kubeba
abiria zaidi ya mmoja, kutokuwa na kadi za pikipiki na kadi za bima,”
alisema Kamanda Sabas.
Kamanda
Salas amesema kuwa wasingeweza kukusanya kiasi hicho cha pesa kwa
kipindi hicho kifupi kama askari polisi wangekuwa wakichukua pesa hizo
kwa maslahi yao wenyewe, ila wamekuwa wakiziingiza katika vitabu vya
Polisi.
Aidha
Kamanda Salas amesema hakuna dereva wa bodaboda anayedaiwa cheti cha
udereva bali wametakiwa kuonyesha leseni zao za udereva kwani ndizo
zinazothibitisha kwamba wamepitia vyuo vya udereva.
Kamanda Salas amewataka madereva
wa bodaboda ambao bado hawajapitia vyuo vya udereva wakajifunze udereva
ndipo waendeshe bodaboda na amewaambia kuwa ili wasikamatwe na askari
polisi basi wasivunje sheria za barabarani.
0 comments:
Post a Comment