Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Rais Dk. John Magufuli leo anatarajiwa kuwasili
mkoani Arusha ambapo keshokutwa atakuwa mgeni rasmi katika sherehe
za kutunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya
Kijeshi cha (TMA), Monduli.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, alisema Dk. Magufuli
atawasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na
amewaomba wananchi kujitokeza kumpokea.
"Nawaomba sana wananchi wa Mkoa wetu kw amara ya kwanza tangu awe rais, ndio anakuja Mkoani kwetu, tujitokeze kumpokea,"alisema.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Mkuu wa Chuo cha
Mafunzo ya Kijeshi cha TMA Meja Jenerali PP Masao, Dk. Magufuli
atatunuku kamisheni kwa maofisa wanafunzi kundi la 57/15.
Alisema Dk. Magufuli atatunuku kamisheni kwa maofisa
wanafunzi kundi hilo, katika sherehe zitakazoanza saa mbili asubuhi
chuoni hapo.
Meja Jenerali Masao alisema wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria sherehe hizo.
Hii ni ziara ya kwanza ya Rais Dk. Magufuli ambaye pia
ni Amiri jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, kufika
mkoani Arusha na pia kutunuku kamisheni, baada ya kuchaguliwa
kushika wadhifa huo Oktoba, mwaka jana.
Katika hatua nyingine, wakuu wa wilaya za mkoa wa
Arusha, zinazokabiliwa na tatizo la ugonjwa wa kipindupindu,
wamewasilisha taarifa ya hatua iliyofikiwa katika kukabiliana na
janga hilo, inayoonyesha kuwa ugonjwa huo sasa umepungua kwa
kiasi kikubwa na uko mbioni kumalizika kabisa.
Wakuu hao ambao ni Fadhili Nkurlu wa wilaya ya Arusha
na Ernest Kahindi wa Longido, walisema kwa sasa katika maeneo
yao, hakuna wagonjwa wapya wa kipindupindu na wameendelea kuwataka
wananchi kuendelea kuzingatia kamuni za usafi.
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment